Shangwe za uzinduzi wa Absa Tanzania Health Club - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Sunday, November 7, 2021

Shangwe za uzinduzi wa Absa Tanzania Health Club

Mmoja wa wakurugenzi wa Benki ya Absa, Esther Maruma akizungumza na wateja na wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa uzinduzi rasmi wa Klabu ya Afya ya wateja maalumu wa Benki ya Absa ambayo kupitia klabu hiyo wateja, familia zao na wafanyakazi wa Absa watapata huduma za afya ya mwili na akili bila gharama kutoka kwa baadhi ya washirika wa Absa na wengine kwa punguzo la bei. Huduma hizo ni pamoja na ushauri na upimaji wa afya, mazoezi ya viungo na elimu ya lishe. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Golden Tulip, Dar es Salaam Jana.
Mteja wa Benki ya Absa, Flavian Kinunda (kulia), akipokea zawadi kutoka kwa mmoja wa wakurugenzi wa Benki hiyo, Esther Maruma wakati wa uzinduzi rasmi wa Klabu ya Afya ya wateja maalumu wa Benki ya Absa ambayo kupitia klabu hiyo wateja, familia zao na wafanyakazi wa Absa watapata huduma za kiafya bila gharama kutoka kwa baadhi ya washirika wa Absa na wengine kwa punguzo la bei. Huduma hizo ni pamoja na ushauri na upimaji wa afya, mazoezi ya viungo na elimu ya lishe. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Golden Tulip, Dar es Salaam Jana.
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Wateja Rejareja wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Lilian Swere (kushoto), akikabidhi zawadi kwa mmoja wa wateja wao, Robert Lowassa mara baada ya tukio la uzinduzi wa Absa health club jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni mmoja wa wakurugenzi wa Absa, Esther Maruma.
Baadhi ya wateja na wafanyakazi wa Benki ya Absa Tanzania wakifanya mazoezi ya yoga yakitolewa na mtaalamu kutoka Mukti, wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Klabu ya Afya ya wateja maalumu wa Benki ya Absa ambayo kupitia klabu hiyo wateja, familia zao na wafanyakazi wa Absa watapata huduma za afya ya mwili na akili bila gharama kutoka kwa baadhi ya washirika wa Absa na wengine kwa punguzo la bei. Huduma hizo ni pamoja na ushauri na upimaji wa afya, mazoezi ya viungo na elimu ya lishe. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Golden Tulip, Dar es Salaam Jana.
Baadhi ya wateja na wafanyakazi wa Absa wakishiriki mbio za kilomita 10 kuashiria Uzinduzi wa Klabu ya Afya ya benki hiyo kwa wateja maalum jijini Dar es Salaam jana.
Mteja wa Benki ya Absa, Flavian Kinunda akipimwa urefu na uzito mhudumu wa Kampuni ya Assemble Insurance wakati wa uzinduzi wa klabu ya afya ya benki hiyo jijini Dar es Salaam jana. Moja ya manufaa ambayo wanachama wa Absa health club watayapata ni kupima afya zao na familia katika Kampuni hiyo.
Baadhi ya wateja, wafanyakazi wa Absa wakipozi mbele ya wapiga picha Mara baada ya kumaliza mbio za kilomita tano na kumi zilizofanyika sambamba na uzinduzi wa Klabu ya Afya ya Absa jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya wateja, wafanyakazi na washirika wa Benki ya Absa wakipozi kwa picha ya kumbukumbu wakati wa uzinduzi wa Klabu ya Afya ya Absa jijini Dar es Salaam jana.

No comments:

Post a Comment

Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu

Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...

Pages