Polisi Wafanya Usafi Stendi Ya Mabasi Arusha - THINKING IN BUSINESS

Mgongopr.blogspot.com is a business centered online platform highlighting trade, finance and economic news in Tanzania. Our coverage is customised to ensure we consolidate brands, boost sales and nurture investments. The site is an imprint of Mgongo Logistics and Solutions, a trusted consultancy firm, offering Social Media Management, Photography, Videography, Advertising, Event Management and Translation. For more information contact us via; Phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Wednesday, January 18, 2023

Polisi Wafanya Usafi Stendi Ya Mabasi Arusha



Na Mwandishi wetu, Jeshi la Polisi.

Jeshi la Polisi Kupitia Kikosi cha Kuzuia Wizi wa mifugo Tanzania (STPU) wameungana na wananchi kufanya usafi wa mazingira katika stendi Kuu ya Mabasi Mkoa wa Arusha.

Kamanda wa Kikosi hicho ambaye aliongoza zoezi hilo, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Simon Pasua amesema wameamua kufanya usafi katika eneo hilo kuonyesha umuhimu wa usafi kwakua watu wengi hufika kwa ajili ya kupata huduma ya usafiri ambapo linapaswa kuwa safi wakati wote.

Kamanda Pasua ameendelea kusema kuwa mbali na kuhakikisha ulinzi wa raia na mali zao pia jeshi hilo linaungana na serikali kuhakikisha raia wake wanakua salama kiafya kwa kuhakikisha mazingira yanakua salama.

Naye Msimamizi wa Stendi hiyo Bwana Humprey Mwarija amesema Polisi ni sehemu ya jamii hivyo kupitia usafi ambao wameufanya utasaidia kwa kiasi kikubwa kuileta jamii karibu na jeshi hilo katika mapambano dhidi ya uhalifu kwani wananchi watakua tayari kutoa ushirikiano katika kutoa taarifa za uhalifu.

Nao baadhi ya wananchi kwa nyakati tofauti mbali na kushukuru jeshi hilo, wamesema ni mara ya kwanza kuona polisi wakifanya shughuli za usafi kwani mara zote wanawaona wakiwa wamebeba silaha hivyo wakaomba taasisi nyingine za ulinzi kuwa karibu wananchi ili kupunguza kuogopwa hali ambayo itasaidiataarifa za uhalifu kupatikana kwa urahisi.

No comments:

Post a Comment

BENKI YA ABSA YAENDELEA KUWAWEZESHA WANAWAKE WAJASIRIMALI KIUCHUMI

Meneja Bidhaa wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Bryton Kimemeta (kushoto), akizungumza na baadhi ya wanawake wajasiriamali, wanachama wa Taasis...

Pages