ROTARY TANZANIA YAENDELEA ILIPOISHIA, SASA NI ZAMU YA WAKAZI WA BUNJU KUPATA MATIBABU BURE - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Thursday, November 16, 2023

ROTARY TANZANIA YAENDELEA ILIPOISHIA, SASA NI ZAMU YA WAKAZI WA BUNJU KUPATA MATIBABU BURE

 

Rais wa Rotary Club upande wa Oystarbay jijini Dar es Salaam Abdulrahman Hussein (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari wakati wakitangaza fursa ya kutoa huduma ya afya na matibabu bure kwa wakazi wa Bunju ikiwa ni muendelezo wa Rotary kusaidia jamii hasa katika sekta ya afya hii imekuwa ni utaratibu wa Rotary kujitolea kuhakikisha wanasaidia watu ambao wanamatatizo mbalimbali ya kiafya na kukosa uwezo wakujitibu. Hafla hiyo hiyo imefanyika leo masaki jijini humo wengime pichani ni Mwenyekiti wa Rotary Tanzania Diamond Carvalho pampja na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Bi Mehreen Khatri.


Mwenyekiti wa Rotary Tanzania Diamond Carvalho (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari wakati wakitangaza fursa ya kutoa huduma ya afya na matibabu bure kwa wakazi wa Bunju ikiwa ni muendelezo wa Rotary kusaidia jamii hasa katika sekta ya afya hii imekuwa ni utaratibu wa Rotary kujitolea kuhakikisha wanasaidia watu ambao wanamatatizo mbalimbali ya kiafya na kukosa uwezo wakujitibu. Hafla hiyo hiyo imefanyika leo masaki jijini humo wengine pichani ni Rais wa Rotary Club upande wa Oystarbay jijini Dar es Salaam Abdulrahman Hussein pamoja na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Bi Mehreen Khatri.


Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Bi Mehreen Khatri(kushoto), akizungumza na waandishi wa habari wakati wakitangaza fursa ya kutoa huduma ya afya na matibabu bure kwa wakazi wa Bunju ikiwa ni muendelezo wa Rotary kusaidia jamii hasa katika sekta ya afya hii imekuwa ni utaratibu wa Rotary kujitolea kuhakikisha wanasaidia watu ambao wanamatatizo mbalimbali ya kiafya na kukosa uwezo wakujitibu. Hafla hiyo hiyo imefanyika leo masaki jijini humo wengime pichani ni Mwenyekiti wa Rotary Tanzania Diamond Carvalho pamoja na Rais wa Rotary Club upande wa Oystarbay jijini Dar es Salaam Abdulrahman Hussein



Mamia ya wakazi wa Bunju na maeneo ya Jirani wametakiwa kujitokeza kwa wingi siku ya Jumamosi Novemba 18 2023 katika viwanja vya shule ya msingi bunju kupima afya zao katika kambi maalum ya afya itakayoendeshwa na Rotary Tanzania.


Rotary ikishirikiana na wadau mbalimbali wa afya na wafadhili, wataendesha huduma hiyo siku nzima ya Jumamosi Novemba 18, ili kuwawezesha wakazi wengi wa Bunju, maeneo ya Jirani na Dar es Salaam kwa ujumla kupata mud awa Kwenda kupima afya zao na kupata ushauri wa kitaalamu bure bila malipo yoyote.


Hayo yameelezwa na Diamond Carvalho, Mwenyekiti wa Rotary Tanzania wakati akizungumza na waandishi wa habari masaki jijini Dar es Salaam alipokuwa akielezea kuhusu maandalizi ya kambi hiyo ya siku moja itakayofanyika Bunju jijini Dar es Salaam.


Inakadiriwa kuwa kuna wanafunzi 3500 na watu wazima 1500 watakaoshiriki, na kila mmoja wao atapata huduma muhimu kama vile vipimo, na elimu ya afya na kinga, uchunguzi wa macho, uchunguzi wa saratani mbali mbali, ukaguzi wa meno, elimu ya hedhi salama, na fursa ya kupata chanjo, dawa na rufaa za wataalamu kama itahitajika.


Kwa moyo wa kujitolea, madaktari takribani 100 wakiwemo madaktari wa kawaida 50 na wataalamu wengine 50 wa meno, Macho, Ngozi, Watoto, na huduma nyingine wameahidi kutoa msaada wao kwa kutoa huduma hizi muhimu wakishirikiana na timu kubwa ya wahudumu takribani 500 inaunga mkono juhudi hizi, na ushirikiano huu unasisitiza umuhimu wa upendo na umoja katika kukabiliana na mahitaji ya afya ya jamii.


Diamond Carvalho, , ameeleza, kuwa “Rotary Tanzania, kwa kushirikiana hasa na Klabu ya Rotary ya Oysterbay, imekuwa ikiandaa kambi za matibabu kwa ushirikiano na Klabu ya Rotaract ya Kairiuki tangu mwaka 2012, lengo likiwa kutoa huduma za afya msingi kwa jamii ya Dar es Salaam. Kampeni ya afya ya leo inaadhimisha hatua muhimu sana, ikiwa imeongezeka mara tatu ukubwa wa kambi za matibabu zilizofanywa hapo awali na klabu yetu.


“Tunapenda kuwashukuru sana Vilabu vya Rotary na Rotaract washirika wetu, vilevile washirika muhimu – Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Awamu ya Sita Ikiongozwa na Raisi Doctor Mama Samia Suluhu Hassan, Wizara ya Afya, Bill & Melinda Gates Foundation, Guaranty Trust Bank, Pepsi, SGA Security, Jollie Pads, Agha Khan Health Service, Manufaa Media, Bakhressa Group ,Chemi Cotex, Hitech Sai Hospitals, Afya Intelligence na Management and Development for Health (MDH).” Amesema Calvalho


Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Mehreen Khatri amesema maandalizi yote yamekamilika na amewashauri wakazi wa Dar es Salaam kutumia fursa hii adhimu kuja na kupima afya zao Pamoja na kupata ushauri na elimu ya afya. “tunashukuru maandalizi yote yamekamilika. Hii ni kutokana na ushiriki mkuwa wa wanachama wa Rotary Tanzania Pamoja wafadhili wetu. Tunaamini watu wengi watajitokeza kupima afya zao siku hiyo” alisema Mehreen.


Naye Abdulrahman Hussein Rais wa Rotary Club ya Osterbay Dar es Salaam amesema Jumla ya wakazi 5000 kutoka Bunju na maeneo ya jirani watapata huduma za afya na elimu bila malipo wakati wa tukio la siku ya Afya ya Rotary inayofanywa kwa ushirikiano na Vilabu vya Rotaract vya Kairuki, Muhimbili, KIUT, Alpha, na Kwanza

No comments:

Post a Comment

Absa Dar City Marathon 2024 zatimua vumbi jijini Dar es Salaam

Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Bwana Aron Luhanga (kushoto), akikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza wa mbio za nu...

Pages