Airtel Tanzania yaifikisha SmartWASOMI kwa walimu wa IT Visiwani Zanzibar - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Sunday, September 21, 2025

Airtel Tanzania yaifikisha SmartWASOMI kwa walimu wa IT Visiwani Zanzibar

Ofisa Vifaa vya Intaneti wa Mradi wa Airtel SmartWASOMI, Bw. Harrison Isdory (kushoto), akitoa maelekezo kuhusu matumizi ya baadhi ya vifaa vya intaneti katika warsha iliyoandaliwa kwa walimu wa IT, mjini Zanzibar hivi karibuni, iliyoandaliwa na Airtel Tanzania kupitia Airtel Africa Foundation, kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Elimu, chini ya mpango wa Airtel SmartWASOMI, unaolenga kuboresha elimu ya kidigitali kwa kuwawezesha walimu na wanafunzi kupata maudhui ya kielimu kupitia maktaba mtandao ya Taasisi ya Elimu Tanzania na Shule Direct bila gharama ya vifurushi vya data.

Airtel Tanzania, kupitia Airtel Africa Foundation na kwa kushirikiana na UNICEF pamoja na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, imeendesha warsha ya mafunzo kwa walimu wa Zanzibar mwishoni mwa wiki, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Airtel SmartWASOMI. Mpango huu wa elimu ya kidijitali unalenga kuongeza upatikanaji wa elimu bora kupitia teknolojia kote nchini Tanzania.

Warsha hiyo iliwaunganisha walimu 36 kutoka shule mbalimbali za sekondari ambazo tayari zimeunganishwa na jukwaa la Airtel SmartWASOMI. Tangu uzinduzi wake mwezi Mei 2024 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, mpango wa Airtel SmartWASOMI umefikia zaidi ya shule 400 na umeleta athari chanya kwa maelfu ya walimu na wanafunzi nchini. Jukwaa hili linatoa huduma ya bure ya mtandao kwa rasilimali muhimu za kielimu, ikiwa ni pamoja na maudhui yaliyoidhinishwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) na Shule Direct, hivyo kuwawezesha walimu na wanafunzi kujifunza bila wasiwasi wa gharama za data.

Mgeni rasmi katika tukio hilo, Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari Zanzibar, Bi. Asia Iddy Issa, alisifu mpango huo na kusisitiza kwamba unakwenda sambamba na malengo ya kitaifa.

Mpango huu unasaidia ndoto yetu ya kuunda kizazi chenye uelewa wa kidijitali na unatatua changamoto zilizokwamisha upatikanaji wa nyenzo bora za kujifunzia, hasa katika maeneo yenye uhitaji mkubwa kwa kuwajengea uwezo walimu na kuondoa kikwazo cha gharama za data, tunapunguza pengo kati ya mbinu za kiasili za ufundishaji na ufundishaji wa kisasa,” alisema Asia.

Akaendeleo kusema, “Tunakaribisha kwa moyo mmoja suluhisho kama hili bunifu, kwani linakamilisha juhudi zetu za kuimarisha mfumo wa elimu kwa njia ya kidijitali, tunatarajia kuona shule nyingi zaidi Zanzibar zikifaidi kupitia Airtel SmartWASOMI, na tumejizatiti kushirikiana na wadau wote kuhakikisha kuna matokeo ya kudumu.

Akizungumza kwa niaba ya Wizara ya Elimu, Mkuu wa Idara ya Elimu ya Sekondari Zanzibar, Mfaume Jaffary Mfaume ambaye pia alifungua warsha hiyo, alisisitiza umuhimu wa kuwaunga mkono walimu katika mabadiliko ya kidijitali.

Warsha hii inawawezesha walimu kutumia kwa ufanisi zana za kidijitali ili kuboresha utoaji wa somo, kurahisisha upangaji wa masomo, na kuleta matokeo bora ya kujifunza, Airtel SmartWASOMI ni njia rahisi, thabiti na jumuishi ya kuwaunganisha walimu na wanafunzi na rasilimali bora za kujifunzia bila gharama za data,” alisema.

Katika warsha hiyo, walimu walipata mafunzo ya vitendo kuhusu namna ya kuvinjari maudhui ya mitaala, kuunganisha rasilimali za kidijitali katika masomo yao, na kufuatilia ushiriki wa wanafunzi kwa ufanisi zaidi. Pia walihimizwa kujifunza kwa kushirikiana, kushirikiana mawazo, na kujenga mtandao wa walimu waliowezeshwa kwa njia ya kidijitali.

Walimu waliohudhuria walielezea shukrani zao kwa Airtel Africa Foundation, UNICEF na serikali kwa kuanzisha mpango unaosaidia mbinu za kisasa, zinazopatikana kwa urahisi na zenye ufanisi katika shule.

Kwa upande wake, Yussuf Mwadini Haji, mwalimu wa Shule ya Sekondari Hamamni, alisema, “Kabla ya warsha hii, wengi wetu hatukujua uwezo mkubwa wa zana za kidijitali. Sasa najisikia kuwa na ujasiri na hamasa ya kufanya masomo yangu yawe ya kuvutia zaidi kwa wanafunzi.

Mwalimu mwingine, Amina Hamza Shaabani kutoka Shule ya Sekondari Forodhani, aliongeza, “Airtel SMARTWASOMI imefungua fursa mpya. Sasa tunapata maudhui ya kisasa bila gharama za data, jambo ambalo limepunguza mzigo mkubwa.

Mafunzo haya ni sehemu ya dhamira pana ya Airtel Tanzania ya kuunganisha zaidi ya shule 1,000 ifikapo mwisho wa mwaka 2025. Kampuni hiI ya mawasiliano inaendelea kuwekeza katika miundombinu ya kidijitali, ushirikiano na jamii, pamoja na kushirikiana kwa karibu na wadau ili kupanua wigo na manufaa ya mpango wa Airtel SmartWASOMI. Mpango huu unachangia moja kwa moja malengo ya taifa ya kuboresha uelewa wa kidijitali, kupunguza pengo la elimu, na kuhakikisha walimu na wanafunzi katika maeneo yote wanapata elimu bora ya kidijitali.
Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari visiwani Zanzibar, Bi. Asia Iddy Issa, akizungumza katika katika warsha iliyoandaliwa kwa walimu wa IT, mjini Zanzibar hivi karibuni, iliyoandaliwa na Airtel Tanzania kupitia Airtel Africa Foundation, kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Elimu, chini ya mpango wa Airtel SmartWASOMI, unaolenga kuboresha elimu ya kidigitali kwa kuwawezesha walimu na wanafunzi kupata maudhui ya kielimu kupitia maktaba mtandao ya Taasisi ya Elimu Tanzania na Shule Direct bila gharama ya vifurushi vya data.
Ofisa Vifaa vya Intaneti wa Mradi wa Airtel SmartWASOMI, Bw. Harrison Isdory (kushoto), na Mratibu wa Elimu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE), Bw. Charles Manyama (kulia), wakiangalia wakati Mwalimu wa Shule ya Sekondari Hammamni ya mjini Zanzibar, Bw. Yussuf Mwadini Haji, akifanya usajili katika mfumo wa TIE, wakati wa warsha iliyoandaliwa kwa walimu hao, visiwani humo, jana, iliyoandaliwa na Airtel Tanzania kupitia Airtel Africa Foundation, kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Elimu, chini ya mpango wa Airtel SmartWASOMI, unaolenga kuboresha elimu ya kidigitali kwa kuwawezesha walimu na wanafunzi kupata maudhui ya kielimu kupitia maktaba mtandao ya Taasisi ya Elimu Tanzania na Shule Direct bila gharama ya vifurushi vya data.
Ofisa Vifaa vya Intaneti wa Mradi wa Airtel SmartWASOMI, Bw. Harrison Isdory (kulia), akizungumza na baadhi ya walimu wa IT mjini Zanzibar, katika warsha iliyoandaliwa kwa walimu hao, na Airtel Tanzania kupitia Airtel Africa Foundation, kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Elimu, chini ya mpango wa Airtel SmartWASOMI, unaolenga kuboresha elimu ya kidigitali kwa kuwawezesha walimu na wanafunzi kupata maudhui ya kielimu kupitia maktaba mtandao ya Taasisi ya Elimu Tanzania na Shule Direct bila gharama ya vifurushi vya data.
Baadhi ya walimu wa IT mjini Zanzibar hivi karibuni, wakiwa katika warsha iliyoandaliwa kwa walimu hao na Airtel Tanzania kupitia Airtel Africa Foundation, kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Elimu, chini ya mpango wa Airtel SmartWASOMI, unaolenga kuboresha elimu ya kidigitali kwa kuwawezesha walimu na wanafunzi kupata maudhui ya kielimu kupitia maktaba mtandao ya Taasisi ya Elimu Tanzania na Shule Direct bila gharama ya vifurushi vya data.

No comments:

Post a Comment

Airtel Tanzania yaifikisha SmartWASOMI kwa walimu wa IT Visiwani Zanzibar

Ofisa Vifaa vya Intaneti wa Mradi wa Airtel SmartWASOMI, Bw. Harrison Isdory (kushoto), akitoa maelekezo kuhusu matumizi ya baadhi ya vifaa ...

Pages