MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AWASHAURI VIONGOZI KUJENGA UTAMADUNI WA KUWASAIDIA WANANCHI - THINKING IN BUSINESS

Mgongopr.blogspot.com is a business centered online platform highlighting trade, finance and economic news in Tanzania. Our coverage is customised to ensure we consolidate brands, boost sales and nurture investments. The site is an imprint of Mgongo Logistics and Solutions, a trusted consultancy firm, offering Social Media Management, Photography, Videography, Advertising, Event Management and Translation. For more information contact us via; Phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Tuesday, March 3, 2026

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AWASHAURI VIONGOZI KUJENGA UTAMADUNI WA KUWASAIDIA WANANCHI

 

Mwakilishi wa Jimbo la Kiwani ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewashauri viongozi kujenga utamaduni wa kuwasaidia wananchi hasa katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani ili kuweka uwiano sawa wa mahitaji.

Ametoa wito huo mara baada ya zoezi la kuwagawa Iftar kwa wananchi wa jimbo la kiwani shehia ya kendwa yenye nyumba zaidi ya 1156 hafla iliyofanyika kwenye uwanja wa mpira wa Mauuwani Jimbo la Kiwani.

Amesema ataendeleza utamaduni wake wa kugawa Iftari kwa wananchi wote hasa wenye mahitaji Maalum ili kupunguza ukali wa maisha na kupata chakula katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Amefahamisha kuwa mwezi Mtukufu wa Ramadhan ni Maalum kwa waumini wa Dini ya kiislamu kufanya matendo mema yanayompendeza Mwenyezi Mungu,hivyo ni vyema kwa kila mwenye uwezo kutoa na kuwapa wahitaji ili kupata fadhila zilizomo ndani ya mwezi huu.

Aidha, Mhe. Hemed amesema anatarajia kuzifikia shehia zote saba ( 7 ) zilizomo ndani ya Jimbo hilo na kuzipatia Iftari jambo ambalo litaongezea umoja na mshikamano kwa wannachi wa jimbo hilo.

Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewaomba wafanya biashara kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu wakiweo Masikini, Wajane, Mayatima na watu wasiojiweza hasa katika mwezi mtukufu wa ramadhani ili kuzidi kuzitakada biashara zao na kupata fadhila zilizomo ndani ya mwezi wa ramadhani.

Kwa upande wake mfanya biashara SAID NASSIR NASOR ( BOBAR ) ameishukuru serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kwa kuendelea kumpatia ushirikiano ambapo kwa mwezi huu wa ramadhani amepatiwa usafiri wa kusafirisha bidhaa mbali mbali ambazo atawakabidhi wananchi wa kisiwani Pemba wakiwemo waannchi wa jimbo la kiwani.

Amesema kuwa lengo lake ni kuwafikia wananchi mbali mbali wasio na uwezo kwa Unguja na Pemba ili kila mwananchi apate sadaka itakayowasaidia kwa Iftari lakini pia aweze kupata fadhila hapa duniani na kesho akhera.

Nao wananchi waliopatiwa sadaka hizo wamemshukuru mwakilishi wao kwa kuendelea kuwatumikia kwa moyo wa upendo, huruma na usawa kwa wananchi wote jimboni humo jambo ambalo linawapa faraja na imani kubwa juu yake.

Wamesema hawana shaka na utendaji kazi wa Mhe. Hemed na matumaini yao makubwa ni kuzidi kuwaletea maendeleo jimbo humo kama vile alivyoanza kuzitekeleza ahadi mbali mbali alizoziahidi wakati akiomba ridhaa ya kuwa mwakilishi wa Jimbo la Kiwani.

No comments:

Post a Comment

ABSA BANK TANZANIA REAFFIRMS COMMITMENT TO WOMEN’S ECONOMIC EMPOWERMENT AS A NATIONAL GROWTH IMPERATIVE

Dar es Salaam, Tanzania, 4 March 2026:  Absa Bank Tanzania has reaffirmed its commitment to advancing women’s economic empowerment, position...

Pages