Benki ya Absa yaungana na TPSF kuwajengea uwezo wanawake wajasiriamali - THINKING IN BUSINESS

Mgongopr.blogspot.com is a business centered online platform highlighting trade, finance and economic news in Tanzania. Our coverage is customised to ensure we consolidate brands, boost sales and nurture investments. The site is an imprint of Mgongo Logistics and Solutions, a trusted consultancy firm, offering Social Media Management, Photography, Videography, Advertising, Event Management and Translation. For more information contact us via; Phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Sunday, June 21, 2026

Benki ya Absa yaungana na TPSF kuwajengea uwezo wanawake wajasiriamali

Meneja Miradi wa Benki ya Absa, Bi. Munira Chambuso akizungumza katika semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa  kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kwa wanawake wajasiriamali wadogo na wa kati, ikihuhusu   elimu ya fedha na  usimamizi wa uwekezaji, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Meneja wa Huduma za Jamii na Matukio wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi akizungumza na baadhi katika semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa  kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kwa wanawake wajasiriamali wadogo na wa kati ikihusu   elimu ya fedha na  usimamizi wa uwekezaji, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi wa Wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bi. Kinanasy Seif akizngumza katika semina iliyoandaliwa na Benki ya Absa Tanzania kwa kushirikiana na taasisi hiyo kwa wanawake wajasiriamali wadogo na wa kati, ikihusu  elimu ya fedha na  usimamizi wa uwekezaji, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Meneja Bidhaa Kitengo cha Biashara wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Devroda Kagusa, akizungumza katika semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa  kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), kwa wanawake wajasiriamali wadogo na wa kati, Ikihusu   elimu ya fedha na  usimamizi wa uwekezaji, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Ofisa Elimu kwa Mlipa Kodi na Mawasiliano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Zephania Mange, akitoa elimu kuhusu wajibu wa mlipa kodi katika semina iliyoandaliwa na Benki ya Absa Tanzania kwa  kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), kwa wanawake wajasiriamali wadogo na wa kati, Ikihusu   elimu ya fedha na  usimamizi wa uwekezaji, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Wawakilishi kutoka Benki ya Absa na TPSF, wakipiga picha ya kumbukumbu pamoja na washiriki wa semina hiyo pamoja na wawezeshaji wengine, mara baada ya kumalizika kwa semina hiyo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Benki ya Absa Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), wameandaa semina wanawake wajasiriamali wadogo na wa kati, kutoka sekta mbalimbali ili kuwajengea uwezo katika elimu ya masuala ya kifedha pamoja na  usimamizi wa uwekezaji, iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.


 Akizungumza wakati wa semina hiyo, Meneja Huduma za Jamii na Matukio wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi alisema  mpango huo ulianza muda mrefu  kama sehemu ya ajenda ya uwajibikaji kwa jamii ya benki hiyo, inayolenga kuwawezesha wananchi, hususan wanawake wajasiriamali, kupata maarifa ya kifedha yatakayowasaidia kuwekeza kwa ufanisi na kuimarisha biashara zao.


 “Tunafurahi kuona wanawake wengi wakishiriki mafunzo haya, elimu inayotolewa inaenda sambamba na lengo la Benki ya Absa la ‘Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, Hatua Moja baada ya nyingine’, tunaamini mafunzo wanayoyapata yatawawezesha katika kufikia mafanikio ya kiuchumi na kuimarisha ustawi wa biashara zao.


 “Sisi hapa tuna ahadi ya chapa yetu isemayo ‘Stori yako ina Thamani’, hivyo tunaposhirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) katika kuwapa wajasiriamali hawa elimu ya kifedha na maarifa mengine ya kibiashara, tunaamini tunaenda kuwasaidia wafanyabiashara hawa kukamilisha stori za mafanikio yao, kwani stori zao zina thamani sana kwetu”, aliongeza Bi. Abigail.

 

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bi. Kinanasy Seif alisema, shirikisho hilo litaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuwawezesha wanawake wajasiriamali kupitia programu za mafunzo na elimu zinazolenga kukuza biashara na kuimarisha uchumi wao.

 

Alisema TPSF imekuwa ikitekeleza programu mbalimbali za kuwawezesha wanawake katika nyanja tofauti za kibiashara huku ikitambua mchango mkubwa wa wanawake katika maendeleo ya sekta binafsi na uchumi wa taifa kwa ujumla.

 

“Tumefanikiwa kuwaleta pamoja wanawake wajasiriamali kutoka maeneo  mbalimbali ili wapate mafunzo ya elimu ya fedha na uwekezaji kutoka Benki ya Absa, tunaamini maarifa haya yatawasaidia kufanya maamuzi sahihi ya kifedha na kukuza biashara zao,” alisema Bi. Kinanasy akiongeza kuwa ushirikiano kati ya TPSF na Benki ya Absa ni hatua muhimu katika kuhakikisha wanawake wanapata fursa za kujengewa uwezo na kufikia maendeleo endelevu katika shughuli zao za kiuchumi.

 

Naye Ofisa Elimu kwa Mlipa Kodi na Mawasiliano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutoka Mkoa wa Kodi wa Kinondoni, Bw. Zephania Mange, alisisitiza umuhimu wa kuzingatia sheria za kodi katika kujenga biashara imara na endelevu pamoja umuhimu wa  walipakodi kutekeleza wajibu wao, na pia kufahamu haki zao wanazostahili kupata kutoka katika mamlaka hiyo.

 

Alisema miongoni mwa haki hizo ni usiri wa taarifa za kikodi, ambapo taarifa zote zinazowasilishwa na mlipakodi zinapaswa kubaki siri na haziwezi kutolewa kwa watu wasiohusika. Aidha, walipakodi wote wanapaswa kuhudumiwa kwa usawa bila upendeleo wowote.

 

“Walipakodi pia wana haki ya kupinga maamuzi yanayotolewa na maafisa wa kodi pale wanapoona hawajaridhika nayo kwani maamuzi ya awali sio ya mwisho, hivyo kuna fursa ya kukata rufaa kwa kufuata taratibu zilizowekwa”, alisema Bw. Mange.

 

Kwa upande wa wajibu wa mlipa kodi, ofisa huyo alisema mamlaka hiyo  inawakumbusha wafanyabiashara kuhakikisha wanajisajili kupata namba ya mlipa kodi (TIN) ndani ya siku tano tangu waanze biashara, na pia wafanyabiashara wanaofikia mauzo yanayostahili kwa mujibu wa sheria wanapaswa kutumia mashine za kutolea risiti za kielektroniki (EFD) ama kujisajili kwenye mfumo wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa waliokidhi vigezo. 

 

No comments:

Post a Comment

Benki ya Absa yaungana na TPSF kuwajengea uwezo wanawake wajasiriamali

Meneja Miradi wa Benki ya Absa, Bi. Munira Chambuso akizungumza katika semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa  kushirikiana na Taasisi ya Se...

Pages