Tuesday, March 1, 2016
![](https://1.bp.blogspot.com/-7Kd9qaiRHuA/WaEtZyc70TI/AAAAAAAADsA/7WUYBVoY-UwwjdEP3kDFPvH9htN0dDKgQCLcBGAs/s1600/demo-image.jpg)
Home
BIASHARA
Benki ya NBC yazindua kitengo kipya cha kuhudumia wateja maalum (Private Banking) mkoani Mwanza.
Benki ya NBC yazindua kitengo kipya cha kuhudumia wateja maalum (Private Banking) mkoani Mwanza.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Mwanza, Elinser Nyange (katikati), akikata utepe
kuashiria uzinduzi wa kitengo maalumu cha kuhudumia wateja maalum (Private
Banking) katika tawi la Benki ya NBC mkoani Mwanza hivi karibuni. Kushoto ni
Meneja wa NBC wa tawi hilo, Godhard Hunja na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha
Wateja Maluum wa NBC, Ashura Waziri. Hiki ni kitengo cha tatu kuanzishwa baada
ya vingine viwili katika matawi ya Sea Cliff na Corporate ya jijini Dar es
Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Maalum wa Benki ya NBC, Ashura Waziri (kulia),
akimpa maelezo Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mwanza,
Elinser
Nyange (katikati) kuhusu huduma za kibenki za NBC wakati wa uzinduzi rasmi wa
kitengo kipya cha kuhudumia wateja maalum (Private Banking) katika tawi la NBC jijini
Mwanza. Hafla hiyo ilifanyika mjini Mwanza hivi karibuni. Anayeangalia ni
Meneja wa tawi hilo, Godhard Hunja. Hiki ni kitengo cha tatu baada ya
vingine viwili kuzinduliwa katika matawi ya Sea Cliff na Corporate ya jijini
Dar es Salaam.
Meneja wa Benki ya NBC tawi la Mwanza,
Godhard Hunja (kushoto), akifafanunua jambo kwa Meneja wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) Mkoa wa Mwanza, Elinser Nyange (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Maalum, Ashura Waziri
akiangalia wakati wa uzinduzi rasmi wa kitengo kipya cha kuhudumia wateja
maalum (Private Banking) katika tawi hilo. Uzinduzi huo ulifanyika mjini Mwanza hivi
karibuni.
Meneja wa Mamlaka ya
Mapato (TRA) Mkoa wa Mwanza, ElinserNyange (wa pili kulia) akifanya mahojiano wa waandishi wa
habari (hawapo pichani) wakati wa hafla hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Minister officially launches real estate giant Coldwell Banker Tanzania and Zanzibar
Zanzibar Minister for Labour, Economy, and Investment, Shariff Ali Shariff addresses guests during the launch of Coldwell Banker Tanzania an...
No comments:
Post a Comment