Halotel wakubaliana na Serikali kujenga minara mipya 47, kufikisha mawasiliano Vijijini - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Friday, August 18, 2017

Halotel wakubaliana na Serikali kujenga minara mipya 47, kufikisha mawasiliano Vijijini


Kampuni ya simu ya Halotel kwa kushirikiana na Serikali imetiliana saini Mkataba wa kuboresha Mawasiliano vijijini baina ya kampuni hiyo na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (USCAF) tukio ambapo Halotel itajenga minara mipya 47 sawa na asilimia 59 ya tenda iliyotolewa kwa makampuni yote ya simu hapa nchini.

UCASAF kusainiwa kwa mikataba hiyo ni moja ya kutekekeleza malengo makuu ya Mfuko huo ambayo ni pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya mawasiliano katika maeneo ya vijijini na maeneo ya mijini yenye mawasiliano hafifu yakifikiwa kwa haraka zaidi hivyo kwa hatua hiyo ya Halotel itawezesha huduma hiyo kufika maeneo hayo.

Lakini pia ni kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi na serikali katika utoaji wa huduma za mawasiliano kwa wote katika maeneo ya vijijini yenye mawasiliano hafifu.


Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel, Le Van Dai, kabla ya kuanza kwa hafla ya kutiliana saini Mkataba wa kuboresha Mawasiliano vijijini baina ya kampuni hiyo na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (USCAF). Katika hafla hiyo kampuni ya Halotel itajenga minara mipya 47 sawa na asilimia 59 ya tenda iliyotolewa kwa makampuni yote ya simu. Pamoja naokatika picha ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (USCAF) Mhandisi. Peter Ulanga.


Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (Katikati) akiwashuhudia Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel, Le Van Dai kwa Pamoja na Mkurugenzi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (USCAF) Mhandisi. Peter Ulanga wakitia saini Mkataba wa kuboresha Mawasiliano vijijini baina ya kampuni hiyo na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (USCAF). Katika hafla hiyo kampuni ya Halotel itajenga minara mipya 47 sawa na asilimia 59 ya tenda iliyotolewa kwa makampuni yote ya simu

No comments:

Post a Comment

Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu

Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...

Pages