Sunday, October 15, 2017
NBC yadhamini maadhimisho ya Siku ya Vicoba nchini
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage
(wa pili kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Bidhaa na Wateja Rejareja wa Benki
ya NBC, Andrew Lyimo alipokwenda kuzindua rasmi maadhimisho ya Siku ya Vicoba
nchini katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam jana ambayo NBC ilikuwa ni
mmoja wa wadhamini ambapo ilizindua akaunti maalumu ya kikundi iitwayo ‘NBC
Kikundi Account’ ili kuwawezesha watanzania kiuchumi. Akaunti inafunguliwa na watu kuanzia watano na kuendelea. Wengine
kutoka kushoto ni, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji (NEEC), Beng`i
Mazana Issa, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB), Japhet
Justine, Mkurugenzi wa Mifuko ya Uwezeshaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji (NEEC),
Edwin Christant na Mkurugenzi wa Uwezeshaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji (NEEC),
Anna Dominick.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage
(kulia), akimsikiliza Meneja Bidhaa za Uwekezaji wa NBC, Dorothea Mabonye (wa
pili kushoto), huku wenzake wakiangalia wakati akitembelea banda la NBC katika
maadhimisho hayo.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage
(kulia), akisalimiana na Ofisa Mauzo wa Benki ya NBC, Witness Leverian
alipokwenda kuzindua rasmi maadhimisho ya Siku ya Vicoba nchini katika Viwanja
vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam jana. NBC ilikuwa ni kati ya wadhamini wa
maadhimisho hayo ambapo imezindua akaunti maalumu ya kikundi iitwayo ‘NBC
Kikundi Account’ ili kuwawezesha watanzania kiuchumi katika kikundi cha watu
kuanzia watano na kuendelea.
Ofisa Mauzo wa
Benki ya NBC, Witness Leverian (kulia), akitoa maelezo kuhusu huduma na bidhaa
za benki hiyo kwa baadhi ya washiriki wa maonyesho ya maadhimisho ya Siku ya
Vicoba nchini katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam jana.
Ofisa Mauzo wa Benki ya NBC, Rosina Simbila (kushoto),
akitoa maelezo kuhusu huduma na bidhaa za benki hiyo kwa baadhi ya washiriki wa
maonyesho ya maadhimisho ya Siku ya Vicoba nchini katika Viwanja vya Mnazi
Mmoja, Dar es Salaam jana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...
No comments:
Post a Comment