Saturday, October 14, 2017
WIZARA YA AFYA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA MAMA NA MTOTO KUFIKIA 2020
Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
katikati akiongea na wakuu wa Idara na vitengo mbalimbali hawapo
pichani wa Wizara ya afya kuhusiana na kuimarisha huduma bora za afya
nchini leo jijini Dar es salaam, wa kwanza kushoto ni Naibu wa wizara
hiyo Dkt. Faustine Ndungulile na wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu wa
Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya. Wakati wa kikao chake na wakuu
hao.
WIZARA
ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto imejidhatiti
kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto mpaka kufikia 2020 ili
kutokomeza vifo vya wajawazito na watoto wachanga .
Hayo
yamesemwa na Waziri wa afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na watoto
Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipokutana na Wakuu wa Idara na vitengo
Mbalimbali kwa ajili ya utambulisho wa Naibu Waziri Dkt. Faustine
Ndungulile katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam.
“Vifo
vya wajawazito vimekua tishio nchini hivyo ni lazima tuimarishe huduma
za afya ya mama na mtoto ili tufikie malengo ya kutokomeza vifo
vitokanavyo na uzazi mpaka kufikia 2020 ili kujenga taifa lenye watu
wenye afya bora” alisema Waziri ummy.
Aidha
Waziri Ummy amesema kuwa katika kuboresha hilo amewaagiza wakuu wa
idara wizara ya afya kushirikiana na mfuko wa bima ya afya nchini(NHIF)
kuona kama kuna uwezekano wa kuanzisha bima ya afya kwa wajawazito kwa
bei nafuu hadi kufikia Julai mosi 2018.
Mbali
na hayo Waziri Ummy amesema kuwa wanamipangilio ya kutokomeza kabisa
tatizo la dawa nchini kwa kuweka mpango mkakati kati ya Bohari Kuu ya
Dawa (MSD) na vituo vitoavyo huduma za afya ili kuepuka tatizo hilo
lisijirudie mara kwa mara .
Kwa
upande wake Naibu Waziri Dkt. Faustine Ndungulile amesema kuwa
ameshukuru kwa kupewa dhamana hiyo na atashirikiana vyema na Waziri
pamoja na watendaji wa Wizara hiyo ili kuleta ufanisi na Huduma bora za
afya nchini.
“Nitashirikiana
na Waziri wangu pamoja na nyinyi watendaji wenzangu katika kusimamia na
kutekeleza sera ya afya ili kuweza kutoa huduma bora za afya kwa
watanzania wote bila ya kujali rika,jinsia wala umri” alisema Dkt.
Ndungulile.
Naye
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema kuwa
wamepokea maagizo hayo amabayo baadhi wameanza kuyatekeleza na mengine
atawahimiza watendaji wake kuendana na kasi ya awamu ya tano ya HAPA
KAZI TU ili kuifikisha nchi katika afya bora.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na watoto Dkt.
Faustine Ndungulile wa kwanza kushoto akiongea na wakuu wa Idara na
vitengo mbalimbali wa Wizara ya afya hawapo pichani kuhusiana na
kuimarisha huduma bora za afya nchini leo jijini Dar es salaam,
katikati ni Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Ummy Mwalimu na kulia ni Katibu
Mkuu Wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya. Alipokutana na wakuu hao.
Baadhi
ya Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali wa Wizara ya afya, Maendeleo ya
jamii,Jinsia, Wazee na watoto wakifuatilia kwa makini maelezo kutoka
kwa Waziri mwenye dhamani hiyo Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na Naibu wake
Dkt. Faustine Ndungulile hawapo pichani wakati wa kikao na wakuu wa
idara hizo leo jijini Dar es salaam.
Wakuu
wa Idara na Vitengo mbalimbali wa Wizara ya afya, Maendeleo ya
jamii,Jinsia, Wazee na watoto wakimpongeza Naibu Waziri wa Wizara hiyo
Dkt. Faustine Ndungulile hayupo pichani mara baada ya kuwapa maelezo
wakati wa kikao na wakuu wa idara hizo leo katika ofisi ndogo za wizara
jijini Dar es salaam.
Baadhi
ya Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali wa Wizara ya afya, Maendeleo ya
jamii,Jinsia, Wazee na watoto wakifuatilia kwa makini maelezo kutoka
kwa Waziri mwenye dhamani hiyo Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na Naibu wake
Dkt. Faustine Ndungulile hawapo pichani wakati wa kikao na wakuu wa
idara hizo leo jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
wa kwanza kulia akiteta jambo na Naibu wake Dkt. Faustine Ndungulile
kushoto mara baada ya kikao na wakuu wa idara hizo leo jijini Dar es
salaam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...
No comments:
Post a Comment