NBC yazindua Mwezi wa Huduma kwa Wateja kwa kuboresha huduma za bidhaa zao kukidhi mahitaji ya wateja. - THINKING IN BUSINESS

Mgongopr.blogspot.com is a business centered online platform highlighting trade, finance and economic news in Tanzania. Our coverage is customised to ensure we consolidate brands, boost sales and nurture investments. The site is an imprint of Mgongo Logistics and Solutions, a trusted consultancy firm, offering Social Media Management, Photography, Videography, Advertising, Event Management and Translation. For more information contact us via; Phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Friday, October 13, 2017

NBC yazindua Mwezi wa Huduma kwa Wateja kwa kuboresha huduma za bidhaa zao kukidhi mahitaji ya wateja.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kushoto), akizungumza na wafanyakazi wa benki hiyo katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa benko hiyo katika Tawi la Corporate jijini Dar es Salaam jana. Mkurugenzi huyo alisema katika maadhimisho hayo NBC imezidi kuboresha ubora wa huduma na bidhaa mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya wateja wao wa kada zote. Kulia ni Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa NBC, James Kinyanyi.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kulia) na Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa NBC, James Kinyanyi wakikata utepe ili kurusha ‘puto’ kuashiria uzinduzi rasmi wa Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa benko hiyo katika Tawi la Corporate jijini Dar es Salaam jana.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha NBC, Ngwitika Mwakahesya akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa NBC jijini Dar es Salaam jana.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kulia), akizungumza waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa benko hiyo katika Tawi la Corporate jijini Dar es Salaam jana.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Neema Rose Singo (kushoto), akibadilishana mawazo na Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa NBC, James Kinyanyi huku baadhi ya maofisa wengine wa NBC wakiangalia katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa benki hiyo katika Tawi la Corporate jijini Dar es Salaam jana. Wengine kutoka kulia ni , Alina Maria Kimaryo, Jane Mbago, Ngwitika Mwakahesya na Irene Peter.
Kaimu MKurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kulia) akmsikiliza kwa makini Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa benki hiyo, James Kinyanyi wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa benko hiyo katika Tawi la Corporate jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakiwa na nyuso za furaha wakati kaimu mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo akizungumza nao.
Baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa Mwezi wa Huduma kwa Wateja jijini Dar es Salaam jana. 
 Baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakipozi kwa picha wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa benki hiyo jijini Dar es Salaam jana.

No comments:

Post a Comment

ABSA BANK TANZANIA REAFFIRMS COMMITMENT TO SUPPORTING TANZANIA’S HEALTH SECTOR

Absa Bank Tanzania Managing Director, Obedi Laiser (right), competes alongside other participants during the 10-kilometre race of the 2026 A...

Pages