Tuesday, January 16, 2018

RC MAKONDA AZIDI KUBORESHA SEKTA YA ULINZI NA USALAMA DAR.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amefanya Ziara katika kampuni ya Dar Coach LTD, na kukagua Maendeleo ya Ukarabati wa Mabasi 11 ya Vyombo vya ulinzi na Usalama ikiwemo Jeshi la Wananchi,Jeshi la Police na Magereza, ambapo ameahidiwa hadi Mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu baadhi yatakuwa yameshakamilika na kukabidhiwa.
Akizungumza mara baadaya kutembelea Kampuni inayofanya Ukarabati wa magari hayo Makonda amesema kuwa zoezi la Ukarabati hayo litasaidia kuboresha mazingira ya kazi kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa kuwa kazi ya Ulinzi na Usalama ni wa Raia na linahitaji mazingira rafiki ya kazi.
Aidha Makonda amedhibitisha kulidhishwa na kasi ya ukarabati wa mabasi hayo ambapo amekishukuru kiwanda cha Dar Coach Ltd kwa uzalendo wa kujitolea kukarabati Magari hayo ili kuongeza ufanisi katika vyombo vya ulinzi na usalama.
"Kama mnavyokumbuka Magari haya ni yale yaliyokuwa Chakavu ambapo kwasasa yapo katika hatua ya mwisho kukamilika ambapo yatafungwa vifaa vya kisasa ikiwemo AC, Chaji ya Simu, TV, Viti, Bodi mpya, Taa, Side mirrors, Tairi, Vioo huku baadhi zikiwekewa Vyoo vya Ndani kwa lengo la kuweka mazingira Rafiki kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama" amesema
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Dar Coach LTD ambayo imejitolea kufanya Ukarabati huo Manmeet Lal amesema kuwa zoezi hilo ni katika kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuimarisha Ulinzi na usalama wa Raia na mali zao kwa ujumla. Pia amemhakikishia Rc makonda hadi mwishoni mwa mwezi huu kumkabidhi magari matano ambayo yameshakamilika.
Hata hivyo kwa upande wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar ea salaam Lazaro Mambosasa,amemshukuru Rc makonda kwa hatua aliyoichukua kusaidia vyombo vya ulinzi na usalama kupitia wadau wake kusaidia kukarabati mabasi hayo ambayo yatasaidia kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akishikana mikono na Meneja Mauzo wa Kampuni ya Babasi ya Scania Hanif Ally,walipokutana wakati Mkuuwa Mkoa alipokwenda kufanya ziara kwenye Kampuni ya Dar Coach LTD, na kukagua Maendeleo ya Ukarabati wa Mabasi 11 ya Vyombo vya ulinzi na Usalama ikiwemo Jeshi la Wananchi,Jeshi la Police na Magereza, ambapo ameahidiwa hadi Mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu baadhi yatakuwa yameshakamilika na kukabidhiwa mwengine (kulia) ni mmoja wa Maofisa wa kampuni ya Scania Deogratias Kabeho.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul MakondaA akishikana mikono na Mmoja wa Maofisa wa Kampuni ya Babasi ya Scania Deogratias Kabeho walipokutana wakati Mkuuwa Mkoa alipokwenda kufanya ziara kwenye Kampuni ya Dar Coach LTD, na kukagua Maendeleo ya Ukarabati wa Mabasi 11 ya Vyombo vya ulinzi na Usalama ikiwemo Jeshi la Wananchi,Jeshi la Police na Magereza, ambapo ameahidiwa hadi Mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu baadhi yatakuwa yameshakamilika na kukabidhiwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akipata maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Dar Coach Ltd Manmeet Lal (Sunny) wakati Mkuuwa Mkoa alipokwenda kufanya ziara kwenye Kampuni hiyo na kukagua Maendeleo ya Ukarabati wa Mabasi 11 ya Vyombo vya ulinzi na Usalama ikiwemo Jeshi la Wananchi,Jeshi la Police na Magereza, ambapo ameahidiwa hadi Mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu baadhi yatakuwa yameshakamilika na kukabidhiwa.
Baadhi ya magari ya vyombo vya ulinzi na usalama ambayo yanaendelea kutengenezwa ambayo yalipelekwa yakiwa yameharibika kabisa
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akizungumza leo wilayani Mkuranga mkoani Pwani wakati alipoenda kukagua magari 11 ya vyombo vya ulinzi na usalama yanayotengenezwa na Kampuni ya Dar Coach.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akipewa maelezo leo na Mkurugenzi wa kampuni ya Dar Coach Manmeet Lal kuhusu hatua waliyofikia katika kufanya matengenezo ya magari 11 ya vyombo vya ulinzi na usalama
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikagua magari 11 ya vyombo vya ulinzi na usalama ambayo yanatengenezwa mabodi yake yaliyokuwa yameharibika.Matengenezo hayo yanafanywa na Kampuni ya Dar Coach Ltd
Tags
# KITAIFA
Share This
Newer Article
Wateja sita wa Benki ya NBC wajinyakulia Suzuki Carry ‘kirikuu’ kampeni ya Malengo
Older Article
WATEJA WA UMOJASWITCH WAIBUKA NA MAMILIONI KUPITIA BAHATI NASIBU
MHE.HEMED ABDULLA AFUNGUA KITUO CHA AFYA CHA UZI NA NG'AMBWA
Hassani MakeroDec 27, 2023Shirika la USAID laipongeza serikali ya Tanzania mafanikio katika miradi ya elimu na afya nchini
Hassani MakeroNov 17, 2023Takwimu sahihi nyenzo muhimu mapambano dhidi ya Ukimwi
Hassani MakeroNov 16, 2023
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amefanya Ziara katika kampuni ya Dar Coach LTD, na kukagua Maendeleo ya Ukarabati wa Mabasi 11 ya Vyombo vya ulinzi na Usalama ikiwemo Jeshi la Wananchi,Jeshi la Police na Magereza, ambapo ameahidiwa...
No comments:
Post a Comment