Mama mjane anayeishi kigamboni Magenge ya juu RUKIA MBARAKA SAID amlilia na kumwomba RC MAKONDA kumsaidia kwani amedhulumiwa kiwanja chake takribani miaka 23 sasa na hajapata haki yake.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mjane huyo amesema amathulumiwa kiwanja A Block 31 kilichopo kigamboni eneo la Ferri ambapo anadai kuwa amedhulumiwa na jirani yake, lakini kodi ya kiwanja hicho wanalipia wao na wananyaraka zote halali za eneo hilo.
"Nimeamua kupaza sauti kuomba msaada kwani sijapata haki yangu na tumeenda mahakama zote tumeshinda lakini hatujapata haki zetu kwani matariji wanatunyonya sisi wanyonge ,nilikuwa sina hata ada ya watoto wangu ambapo walifukuzwa shule lakini sasa kutokana na msaaada wa Rais wetu elimu bure ndipo karudi shule ,sisi tunalipa kodi ya eneo hili tokea mwaka 1986 hadi sasa lakini sijapata haki"Amesema Rukia Saidi.
Ameeleza kuwa wamefuatilia kesi hiyo mahakama zote wakashinda kesi hiyo lakini hawajapatiwa haki yao amesema ameamua kupaza sauti kwani amehangaika kwa miaka yote bila ya mafanikio na aliposikia tangazo la Mkuu wa mkoa wa dar es salaam la kuwasidia wanyonge wote waliodhulumiwa mali zao ndipo alipoamua kulifika ila kwa kuchelewa anaamini haki yake itapatikana .
"Mimi mjane nahangaika tangu mwaka 1995 na sijapata haki yangu na nimedhulumiwa eneo langu lililopo Kigamboni Ferri kesi naambiwa imeisha, hivyo Naamini Mhe Paul Makonda Mkuu wa mkoa chini ya Serikali ya Rais wetu John Magufuli tutapata msaada na kupata haki yetu kwani mimi ni mjane na nina watoto 6 ambao wananitegemea"Amesema RUKIA SAIDI.
Amesema kuwa eneo hilo amedhulumiwa na Michael Kagembe na Muhammad Ntundu ambapo wanamiliki eneo hilo bila ya kuwa na nyaraka halali na wameweza kuweka mnara katika eneo hilo na wanaingiza fedha lakini hawalipi kodi ya eneo hivyo amewataka kama wananyaraka halali za eneo hilo basi wawe wanalipa kodi ya eneo na waziwasilishe ili haki iweze kuonekana.
Naye Yahaya Mbaraka amesema eneo hilo ni mali yao ambapo walikuwa wanamiliki tokea mwaka 1986, lakini wamedhulumiwa na watu hao na wameweza kuwasilisha makama za KISUTU hadi mahakama Kuu na wakaweza kushinda kesi lakini hawakuweza kuona haki yenyewe hadi sasa.
"Hawa watu wanasema hili eneo ni lao na wakati hawana nyaraka zozote zinazoonyesha uhalali wa eneo hilo na tumeenda Mahakama ya Kisutu tukashinda na mahakama kuu tukashinda ila wao walikata rufaa ya mahaka ya rufaa ambapo tulipewa majibu kuwa wameshinda kesi bila ya sisi kufika mahakamani hapo tunaomba Mhe. Makonda atusaidi tupate haki yetu" Amesema Yahaya Mbaraka.
No comments:
Post a Comment