Wanawake, Vijana katika halimashauri ya Manispaa ya Ilala wapewa wito - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Monday, February 26, 2018

Wanawake, Vijana katika halimashauri ya Manispaa ya Ilala wapewa wito





Afisa Uhusiano wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala  Tabu Shaibu, (kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini dar es salaam, alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika halimashauri hiyo kwa miezi sita (kushoto) ni Afisa habari wa halmashauri hiyo George Mwakyembe

Afisa Uhusiano Halmashauri ya Manispaa ya Ilala  Tabu Shaibu akizungumza na waandishi wa habari leo jijini dar es salaam,na kutoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika halimashauri hiyo kwa miezi sita.


Katika utekezaji wa miradi ya maendeleo katika halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam kwa mwaka 2017,wameweza kutumia Kiasi cha shilingi 5,544,591 kwa kipindi cha miezi sita mwezi Julai hadi  Desemba katika kutekeleza miradi mbalimbali.

Akizungumza leo na waandishi wa habari Afisa Uhusiano halmashauri ya Manispaa hiyo Tabu Shaibu amesema miradi mbalimbali kwa kipindi kilichoanza Julai hadi Desemba 2017, imeweza kutekelezwa vyema ambapo halmashauri hiyo imeweza kutekeleza  miradi ya Miundo mbinu ya Elimu, miundo mbinu ya barabara, mradi wa maji,ukarabati wa Majengo pamoja na ulipaji wa fidia, ukarabati wa nyumba ya mwalimu pamoja na kuboresha huduma za Afya.

"Katika kipindi cha miezi sita mwezi Julai hadi Desemba, 2017 halmashauri ya Manispaa ya Ilala imepeleka jumla ya shilingi 8,524,000,000/= kwa ajili ya Utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kufikia Desemba kiasi cha shilingi. 5,544,684,591 zimeshatumika katika kuboresha miradi hiyo "Amesema Tabu. 

Ameeleza kuwa halmashauri imeweza kutekeleza miradi inayohusisha Ujenzi wa vyamba vya madarasa,vyoo,na hosteli kwa upande wa shule za msingi wamejenga shule mpya zipatazo 4 kutokana na ongezeko la wanafunzi  pamoja na kujengwa kwa madarasa yapatayo 28.

Ameendelea kusema kuwa shule mpya zilizojengwa ni Kudugala katika kata ya Chanika, Zavala  kata ya Buyuni, Uamuzi Kata ya Majohe na Kinyamwezi kata ya Pugu, pia ametaja shule zilizojengwa madarasa ambazo ni shule za msingi Bonyokwa, Mongo la Ndege Mbondole, Mji mpya, Kibanga,Bangulo, pamoja na shule ya Misitu. 

Pia halmashauri imeweza kujenga matundu ya vyoo katika shule 96 na  katika shule za Buyuni Bwawani Tungini na Kilimani wameweza kujenga matundu 40,  sambamba na kukarabati nyumba ya walimu iliyopo katika shule ya Sekondari Kimanga hii ni kutekeleza mradi wa miundombinu ya Elimu katika halmashauri hiyo. 

Amesema kwa upande wa huduma za Afya halmashauri imekarabati Majengo ya huduma za Mama na Mtoto katika Zahanati ya Msongola pamoja na Mvuti lengo likiwa ni kupunguza vifo vya Mama na Mtoto. 

Aidha Afisa Uhusiano halmashauri ya Manispaa hiyo ametoa rai kwa wanawake,walemavu  pamoja  na vijana kufika katika ofisi za wilaya hiyo kwa lengo la kupata maelekezo ya kupata mikopo kwa ajili ya maendeleo na kuweza kuikwamua kiuchumi. 

"Katika mradi wa Uwezeshaji wanawake walemavu pamoja na vijana halmashauri imepeleka Sh.543,400,000/= kwa mikopo ya wanawake ,vijana pamoja na walemavu hivyo ni fursa kwenu kijitokeza kufika kuuliza namna ya kupata mkopo huo lengo likiwa ni kujikwamua kiuchumi kupitia miradi mbalimbali katika halmashauri"Amesema Tabu Shaibu.

No comments:

Post a Comment

Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu

Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...

Pages