WATEJA WA AIRTEL WAJIZOLEA ZAWADI - THINKING IN BUSINESS

Mgongopr.blogspot.com is a business centered online platform highlighting trade, finance and economic news in Tanzania. Our coverage is customised to ensure we consolidate brands, boost sales and nurture investments. The site is an imprint of Mgongo Logistics and Solutions, a trusted consultancy firm, offering Social Media Management, Photography, Videography, Advertising, Event Management and Translation. For more information contact us via; Phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Wednesday, February 7, 2018

WATEJA WA AIRTEL WAJIZOLEA ZAWADI



Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando (katikati) akiongea na waandishi wa habari wakati wakuchezesha droo ya kwanza ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti ambapo washindi 2000 kila mmoja alijishindia 1GB. (Kushoto) ni ni Msimamizi  kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Abdallah Hemedy na Afisa Masoko wa Airtel Nassoro Abubakar. (Picha na Brian Peter)

Promosheni ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti ilizinduliwa mapema wiki hii ambapo kuna washindi 1,000 wakila siku ambao wanajishindia bando ya 1GB pamoja na zawadi nyingine kemkem zikiwepo simu za kisasa za smatiphone na modem za kisasa.

Akiongea baada ya droo hiyo, Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema wateja 2000  wa Airtel wameweza kujishindia bando ya 1GB. 

Kama mnvyoona hapa leo droo ya promosheni yetu ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti imefanyika leo kwa uwazi na washindi wetu wameweza kutoa shukrani na kutuhakikishia kuwa wataendelea kutumia mtandao wetu makini na bora  wa Airtel, alisema Mmbando.

Ni muhimu kufahamu kuwa mteja haitaji kujisajili kwa ajili ya promosheni ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti. Kile anachotakiwa kufanya ni kupiga *149*99# halafu chagua namba 5 Yatosha SMATIKA Intaneti, hapo utanunua bando aidha ya siku, wiki au mwezi na kuwa mmoja wa washindi wa zawadi zetu kabambe, aliongeza Mmbando.

No comments:

Post a Comment

APeF Yazindua Mfuko wa Ziada Kupanua wigo wa uwekaji Akiba, Uwekezaji na Ulinzi

  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, (CMSA), CPA Nicodemus Mkama, akikabidhi waraka wa ofa kwa Kaimu Mwenyekiti ...

Pages