Akiongea na wananchi wa eneo hilo,baada ya uzinduzi wa upimaji, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Alli Hapi amesema amefurahishwa sana kwa mgogoro huu uliogharimu maisha ya watu kumalizika kwa kiwango na manufaa makubwa yenye tija kwa Taifa letu.
Amesema migogoro kama hii imekuwa changamoto kubwa ya amani katika Nchi yetu, hasa Wilaya ya Kinondoni inayohitaji hekima, busara, majadiliano ya kina, na masikilizano katika utatuzi wake.
Akitoa taarifa ya upimaji wa viwanja hivyo Mkurugenzi kutoka kampuni ya Afro Map Ltd iliyoendesha zoezi hilo la upimaji Ndg Fransis Mkwela amesema wamefanikiwa kupima maeneo ya wazi, maeneo ya shule ya Sekondari, maeneo ya viwanda vidogo vidogo, na maeneo ya nyumba za kuabuduia.
Maeneo mengine ni kituo cha polisi, maeneo ya Umma, eneo la kituo cha Afya, eneo la zahanati na eneo la shule ya Msingi.
Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyakasangwe Ndg Peter Belebela akimkaribisha Mkuu huyo wa Wilaya kwenye uzinduzi huo ameushukuru uongozi mzima kwa jitihada zilizofanyika kumaliza mgogoro huo na kuwataka wanachi wake kuheshimu zoezi hilo lá upimaji unaoendelea pamoja na miundo mbinu ya barabara na mipaka.
Mkutano huo umefanyika katika eneo la shule ya Msingi Nyakasangwe uliohusisha wananchi wa eneo hilo pamoja na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali.
No comments:
Post a Comment