Mabasi ya Mwendokasi yasitisha huduma zake kwa muda - THINKING IN BUSINESS

Mgongopr.blogspot.com is a business centered online platform highlighting trade, finance and economic news in Tanzania. Our coverage is customised to ensure we consolidate brands, boost sales and nurture investments. The site is an imprint of Mgongo Logistics and Solutions, a trusted consultancy firm, offering Social Media Management, Photography, Videography, Advertising, Event Management and Translation. For more information contact us via; Phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Sunday, April 15, 2018

Mabasi ya Mwendokasi yasitisha huduma zake kwa muda




Kampuni inayotoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (UDART) imeamua kusitisha usafirishaji wa abiria kwa baadhi ya njia kuanzia saa 11:00 alfajiri kutokana na kufungwa kwa barabara ya Morogoro eneo la Jangwani kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART, Deus Bugaywa na kusema wamechukua maamuzi hayo kutokana na maji mengi ya mvua kupita juu ya daraja la Mto Msimbazi Jijini Dar es Salaam hali ambayo inahatarisha usalama wa abiria na vyombo vya usafirishaji.

"Kwa sasa huduma zinatolewa kwa njia za Kimara - Morroco, Kimara - Magomeni Mapipa, na Gerezani - Muhimbili. Huduma kamili zitarejea mara baada ya barabara kufunguliwa", amesema Bugaywa.

Kwa upande mwingine, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART, Deus Bugaywa amewaomba radhi wananchi wanaotumia usafiri huo kwa usumbufu ambao umejitokeza.

No comments:

Post a Comment

DCB YAZINDUA KAMPENI YA "TUMA BURE, SHINDA KILA WIKI" KUVUTIA WATEJA WA HUDUMA ZA KIDIJITALI

   DAR ES SALAAM: Benki ya DCB imezindua kampeni maalum ya miezi sita ijulikanayo kama " Tuma Bure, Shinda Kila Wiki ", inayolenga...

Pages