NBC YAWASHUKURU WAFANYAKAZI WAKE KWA KUKAMILISHA ZOEZI LA UUZAJI WA HISA ZA VODACOM KWA MAFANIKIO - THINKING IN BUSINESS

Mgongopr.blogspot.com is a business centered online platform highlighting trade, finance and economic news in Tanzania. Our coverage is customised to ensure we consolidate brands, boost sales and nurture investments. The site is an imprint of Mgongo Logistics and Solutions, a trusted consultancy firm, offering Social Media Management, Photography, Videography, Advertising, Event Management and Translation. For more information contact us via; Phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Wednesday, April 18, 2018

NBC YAWASHUKURU WAFANYAKAZI WAKE KWA KUKAMILISHA ZOEZI LA UUZAJI WA HISA ZA VODACOM KWA MAFANIKIO

Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi (wa nne kushoto), akipiga picha na baadhi ya mameneja wa matawi ya NBC katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kuwapongeza na kutambua mchango wa wafanyakazi na matawi yake yaliyfanya vizuri katika kufanikisha uuzwaji wa hisa za awali za Vodacom Tanzania (IPO), na hatimaye kuingizwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mkrugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi (kulia), akikabidhi cheti cha shukurani kwa Mkurugenzi wa Fedha wa Vodacom Tanzania, Jacques Marais  ambapo kwa ushirikiano wa pande zote mbili kulisababisha  kukamilika kwa zoezi hilo lililovunja rekodi katika historia ya Soko la Hisa la Dar es Salaam ambapo zaidi ya watanzania 40,000 walijitokeza kununua hisa  za Vodacom huku NBC ikipewa jukumu la kuhakikisha kuwa mauzo yote ya hisa hizo yanapitia katika benki hiyo na kuhakikiwa. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kushoto), akikabidhi cheti kwa mmoja wa wafanyakazi wa benki hiyo, Salama Mussa katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kuwapongeza na kutambua mchango wa wafanyakazi wake waliohusika kufanikisha uuzwaji wa hisa za awali za Vodacom Tanzania na hatimaye kuingizwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Benki ya NBC Tanzania, Flora Mollel (kushoto), akikabidhi cheti kwa Mariam Kombo, Meneja wa Tawi la NBC Corpoate, katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kuwapongeza na kutambua mchango wa wafanyakazi wake waliohusika kufanikisha uuzwaji wa hisa za awali za Vodacom Tanzania na hatimaye kuingizwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mkuu wa Kitengo cha Makampuni wa NBC, Linley Kapya (kushoto), akikabidhi cheti kwa Noelina Kivaria katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kushoto), akikabidhi cheti kwa mmoja wa wafanyakazi wa benki hiyo, Jacqueline Sindano katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kuwapongeza na kutambua mchango wa wafanyakazi wake waliohusika kufanikisha uuzwaji wa hisa za awali za Vodacom Tanzania na hatimaye kuingizwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Benki ya NBC Tanzania, Flora Mollel (kushoto), akikabidhi cheti kwa Fautina Maeda, Meneja wa Tawi la NBC Samora,  katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kuwapongeza na kutambua mchango wa wafanyakazi wake waliohusika kufanikisha uuzwaji wa hisa za awali za Vodacom Tanzania na hatimaye kuingizwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment

APeF Yazindua Mfuko wa Ziada Kupanua wigo wa uwekaji Akiba, Uwekezaji na Ulinzi

  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, (CMSA), CPA Nicodemus Mkama, akikabidhi waraka wa ofa kwa Kaimu Mwenyekiti ...

Pages