
Mkuu wa mkoa Dar es salaam Paul Makonda amekutana na Balozi wa Ufaransa nchini na kujadili kuhusu kongamano la uchumi litakalofanyika mapema jumatatu wiki ijayo.
Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Rc Makonda amemshukuru balozi huyo na kueleza kuwa wamekuwa marafiki wazuri na Serikali ya Tanzania.

Ameeleza kuwa makampuni hayo yataangalia fursa na vipaumbele vya serikali watakavyovitumia katika kuleta maendeleo na ametoa rai kwa wafanyabiashara wa jiji la Dar es salaam kuja katika ofisi za Mkuu wa Mkoa kujifunza na kuunganishwa na wafanyabiashara hao kutoka ufarasa ili waweze kujifunza na kujenga urafiki katika masoko ya bidhaa zao.
Naye Balozi wa Ufaransa nchini Federic Clavier amefurahi na kumshukuru mkuu ya Mkoa Dar na kueleza kuwa Dar ni mji unaoendelea kukua kiuchumi sambamba na dhamira ya Rais Magufuli ya kufikia uchumi wa kati kufikia mwaka 2025.
Amesema mkutano huo utakuwa na faida baina ya nchi hizi mbili hasa katika kubadilishana teknolojia katika sekta mbalimbali hasa kwa kuangalia afya, maji pamoja na miundombinu na amehaidi matokeo mazuri yenye faida kwa nchi hizo.

No comments:
Post a Comment