Meya wa Wilaya ya
Temeke Abdallah Chaurembo (kushoto),akikabidhi Bendela
ya Taifa kwa vijana Mbwana Abdala, kutoka Kaskazini pemba ( wanne
kulia),
na Shujaa Suleiman kutoka Morogoro, (wa kwanza kulia) kwaajili ya kwenda
kuiwakilisha inchi
katika mashindano ya Afrika yatakayofanyika jumapili ambapo Mgeni Rasmi
anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.
Kasasim
Majaliwa, wanne kushoto ni Msimamizi wa Mashindano hayo Sheikh Nurdeen
Kishk pampoja na viongozi wengine wa dini hiyo, Hafla hiyo
imefanyika viwanja vya shule ya
Al-HIKMA jijini hapa leo.

Msimamizi wa Mashindano ya kusoma na Kuhifadhi Qur-aan Tukufu, Sheykh Nurdeen Kishk,
(watatu kushoto)akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukabidhi Bendela ya Taifa
kwa vijana wa kitanzania waliofuzu mashindano hayo kwaajili ya kwenda
kuwakilisha nchi katika mashindano ya Afrika, ambayo yatafanyika jumapili
katika viwanja vya Taifa jijini Dar es Salaam ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa
kuwa Mh.Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kasasim Majaliwa, (wa
pilikushoto), ni Meya wa Wilaya ya
Temeke Abdallah Chaurembo, (kulia) ni
Mwenyekiti wa Mapambo na ukumbi wa Mashindano hayo Haruna Jumanne, pamoja na Mwenyekiti wa Maulamaa wTanzania, Sheykh Suleyman Kilemile. Hafla hiyo
imefanyika viwanja vya shule ya
Al-HIKMA jijini hapa leo.
Watanzania wawili leo Mei 24 wamekabidhiwa bendera ya taifa ili
kuiwakilisha nchi katika mashindano makubwa ya 19 ya kusoma na kuhifadhi
Qur-aan tukufu Afrika.
Akikabidhi bendera hiyo Meya wa manispaa ya Temeke Abdallah Chaulembo
kwa wawakilishi pekee ambao ni Shujaa Sulemani kutoka Morogoro na Mbwana
Dadi kutoka Pemba amesema kuwa imezoeleka mara nyingi bendera yetu
wanakabidhiwa timu za mpira, lakini leo imekuwa tofauti kwa vijana hawa
kupata fursa adhimu kama hii.
"Napenda kushukuru taasisi ya Al-Hikma kwa kuandaa mashindano haya
ambayo yatakuwa chachu kwa watanzania kuonesha uwezo na kipaji cha
kusoma na kuhifadhi Qur-aan tukufu" amesma Chaulembo
Pia ametoa wito kwa watanzania wote kufika uwanja wa taifa kwa wingi
siku ya mei 27 mwaka huu kushuhudua mashindano hayo ambapo hakuna
kiingilio chochote na mgeni rasmi anatarajia kuwa ni Waziri Mkuu Kassimu
Majaliwa.
Msimamizi wa Mashindano ya kusoma na Kuhifadhi Qur-aan Tukufu, Sheykh Nurdeen Kishk,
Kwa upande wake msimamizi wa mashindano hayo Sheikh Nurdeen Kishk
amesema kuwa washiriki wamepatika kihalali kutoka maeneo yote ya
Tanzania kwani ulifanyika mchojo kwa bila upendeleo.
Aliongeza kuwa mashindano haya yatashirikisha nchi 16 kutoka bara la
Afrika huku kuanzia kesho kukitarajiwa kupokea washiriki na wageni
kutoka sehemu mbalimbali ikiwemo Uingereza, Uganda, Afrika Kusini, Saudi
Arabia, Omani na Kenya.
"Katika kinyang'anyilo hicho mimi na wewe hatujui mshindi wa kwanza
atakuwa nani na atatoka nchi gani ambae atapata kitika cha fedha
kipatacho milioni 15 kikubwa Watanzania wote tufike siku ya tarehe 27
kuona nini kitatokea" amesema Sheikh Kishk
Nae Rais wa taasisi hiyo Sheikh Sharif Abdulkadir ameipongeza Serikali
kwa kitendo cha kulinda amani ya nchi kuonesha ushirikiana kuanzia hatua
ya mwanzo hadi sasa kwani bila amani huwezi kuandaa mashindano kama
haya na kupata washiriki kutoka nchi tofautitofauti kuja kushiriki.
Mwenyekiti wa Mapambo na ukumbi wa Mashindano hayo Haruna Jumanne akizungumza katika hafla hiyo.
Meya wa Wilaya ya
Temeke Abdallah Chaurembo akizungumza katika hafla hiyo
Rais wa taasisi hiyo Sheikh Sharif Abdulkadir akizungumza katika hafla hiyo,
No comments:
Post a Comment