Rc Makonda - TARURA kwa hili tutatwangana mangumi - THINKING IN BUSINESS

Mgongopr.blogspot.com is a business centered online platform highlighting trade, finance and economic news in Tanzania. Our coverage is customised to ensure we consolidate brands, boost sales and nurture investments. The site is an imprint of Mgongo Logistics and Solutions, a trusted consultancy firm, offering Social Media Management, Photography, Videography, Advertising, Event Management and Translation. For more information contact us via; Phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Wednesday, May 9, 2018

Rc Makonda - TARURA kwa hili tutatwangana mangumi





Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewaonya wakandarasi wenye tabia ya kutengeneza Barabara za chini ya kiwango na kuharibika ndani ya muda mfupi jambo linalosababisha hasara kwa serikali na usumbufu kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri. 

Makonda ametoa onyo hilo wakati wa hafla ya  utiaji wa saini kwa Mikataba Nane ya mradi wa matengenezo ya Barabara, Mifereji ya Maji na Culvets inayotekelezwa na Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini TARURA yenye tahamani ya zaidi ya Billion 5.8 ambapo amewataka TARURA kuhakikisha wanasimamia ipasavyo ujenzi wa barabara hizo.

Aidha amezitaja Barabara zitakazojengwa kupitika mradi huo kuwa ni pamoja na Tegeta Nyuki, Msasani, Magomeni Makuti,Migombani, Kimara baruti, Kibanda cha Mkaa, Sheikh Bofu, Kwa Komba, Msigani, Sea clif na Mwananyamala Kisiwani.

Hata hivyo ametoa wiki mbili kwa TARURA kuhakikisha wakandarasi waliojenga barabara chini ya kiwango zinajengwa upya kwa gharama ya mkandarasi ikiwemo barabara ya Mabatini ambapo barabara hizo zitakuwa na mifereji ya maji, sehemu za watembea kwa miguu na Taa za Barabarani. 

Pamoja na hayo  Makonda amesema katika uongozi wake hawezi kufumbia macho matumizi mabovu ya fedha za walipa kodi hivyo atahakikisha anasimama kidete kuhakikisha Dar es salaam inakuwa na barabara zenye ubora.


Sanajari na hayo  Makonda ametaka uwepo wa ushirikiano wa kikazi baina ya TARURA, TANROAD, TANESCO, DAWASCO na TTCL ilikupunguza ucheleweshaji wa miradi na ujenzi usiofuata taratibu unaopelekea uharibifu wa miundombinu.

No comments:

Post a Comment

APeF Yazindua Mfuko wa Ziada Kupanua wigo wa uwekaji Akiba, Uwekezaji na Ulinzi

  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, (CMSA), CPA Nicodemus Mkama, akikabidhi waraka wa ofa kwa Kaimu Mwenyekiti ...

Pages