Monday, May 28, 2018

RESPECT BARBER SHOP IMEANDAA FUTARI KWA WAKAZI WA DAR
Ukizungumzia moja ya mameneja wenye majina makubwa kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva na Dansi hapa nchini, huwezi kuacha kutaja jina la Mohamed Kiumbe ‘Chief kiumbe’ jana amefuturisha jijini Dar es salaam katika ofisi za Respect Barber Shop Kinondoni ambapo mamia ya watu walihudhuria katika futari hiyo wakiwemo wasanii. mbalimbali wa bongofleva na filamu.
Pia Respect Barber Shop imeamua kuandaa futari hiyo kwa wakazi wa jiji hilo ili kuonesha upendo pia kama moja ya sadaka katika mwezi huu mtukufu wa ramadhani.
Baadhi ya wasanii waliohudhuria Iftari hiyo ni pamoja na Khadija Kopa, Mwajuma Abdul ‘Queen Darling’ na Bonge la Nyau na wengine wengi wakiwepo wasanii wa dansi.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Iftari hiyo, Msemaji wa saluni ya Respect, Dakota Delavida amesema kuwa huu ni mwanzo tu ila Mungu akiwapa uzima wataongeza wigo wao kwani ni kitendo cha kurudisha fadhila kwa jamii.
“Chakula ni sadaka na huwezi kupanga kiishie hapa tulijipanga vya kutosha, hii ni mara yetu ya kwanza mwenyezi Mungu akitujaalia uzima tutafanya tukio kama hili tena kwani ni kurudisha fadhili kwa jamii tunayoihudumia” alisema Dakota.
Tags
# BIASHARA
Share This
Newer Article
SERIKALI KUANZISHA CHANJO MPYA YAKUKINGA SARATANI
Older Article
MKOMBOZI BENKI SASA YATOA GAWIO LA HISA
AKIBA COMMERCIAL BANK YAJIKITA KUTOA ELIMU YA KIFEDHA KWA WAJASILIAMALI WADOGO NA WAKATI.
kilole mzeeApr 13, 2025AKIBA COMMERCIAL BANK YAPELEKA TABASAMU KWA WATOTO WANAOLELEWA CHAKUWAMA.
Hassani MakeroMar 28, 2025SIMTANK TANZANIA YATOA ZAWADI KWA MAWAKALA WAKE WAKISHEREHEKEA MIAKA 35 TANGU KUANZISHA
kilole mzeeMar 02, 2025
Labels:
BIASHARA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Ukizungumzia moja ya mameneja wenye majina makubwa kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva na Dansi hapa nchini, huwezi kuacha kutaja jina la Mohamed Kiumbe ‘Chief kiumbe’ jana amefuturisha jijini Dar es salaam katika ofisi za Respect Barbe...
No comments:
Post a Comment