Thursday, May 3, 2018
SHANGWE ZA UZINDUZI WA COPA UMISSETA ZANZIBAR
Mashindano ya shule za sekondari ya Copa Umisseta, yalizinduliwa Zanzibar kwa shamrashamra mbalimbali za michezo na burudani katika uwanja wa Aman na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali,wadau wa michezo na wanafunzi wa shule za sekondari na mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohamed Mahmoud.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, alisema suala la michezo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inalipa kipaumbele kikubwa kwa kuwa inaamini kuwa inayo faida nyingi baadhi yake ikiwa ni kujenga afya,kuleta umoja,burudani na inazo fursa kubwa za ajira hususani kwa vijana na aliipongeza kampuni ya Coca-Cola kwa kuwa mstari wa mbele kudhamini mashindano haya.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohamed Mahmod akipokea zawadi ya mpira wa kufanyia mazoezi kutoka Coca-Cola baada ya hafla ya uzinduzi.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Maghribi, Ayoub Mohamed Mahmod (wa tatu kulia) akikabidhi jezi na mpira kwa mwalimu Mussa Abdi Khamis wa shule ya sekondari ya penae.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud, akipiga mpira kuashiria uzinduzi wa mashindano ya Copa UMISSETA.
Moja ya timu ikikaguliwa wakati wa uzinduzi huo.
Wananchi wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi.
Tags
# SPORTS AND ENTERTAINMENT
Share This
SPORTS AND ENTERTAINMENT
Labels:
SPORTS AND ENTERTAINMENT
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
APeF Yazindua Mfuko wa Ziada Kupanua wigo wa uwekaji Akiba, Uwekezaji na Ulinzi
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, (CMSA), CPA Nicodemus Mkama, akikabidhi waraka wa ofa kwa Kaimu Mwenyekiti ...
No comments:
Post a Comment