SHULE YA KIMATAIFA TANGANYIKA ILIYOPO UPANGA DAR YAWAKUMBUKA WALIOKUMBWA NA MAFURIKO - THINKING IN BUSINESS

Mgongopr.blogspot.com is a business centered online platform highlighting trade, finance and economic news in Tanzania. Our coverage is customised to ensure we consolidate brands, boost sales and nurture investments. The site is an imprint of Mgongo Logistics and Solutions, a trusted consultancy firm, offering Social Media Management, Photography, Videography, Advertising, Event Management and Translation. For more information contact us via; Phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Thursday, May 3, 2018

SHULE YA KIMATAIFA TANGANYIKA ILIYOPO UPANGA DAR YAWAKUMBUKA WALIOKUMBWA NA MAFURIKO

WhatsApp%2BImage%2B2018-05-02%2Bat%2B18.04.12
SHULE ya Kimataifa  Tanganyika iliyopo Upanga wilayani Ilala jijini Dar es Salaam imetoa msaada wa nguo kusaidia wananchi waliokumbwa  na mafuriko.

Msaada huo ulitolewa na Mwasisi wa Shule hiyo Ally Dewji ulipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema ofisini kwake jana. 

Akizungumza mara baada kukabidhi msaada huo Dewji amesema shule yao ya Tanganyika inafundisha watoto wa miaka minne hadi 12, mara baada kutokea mafuriko hayo wanafunzi wa shule hiyo waliguswa. 

"Wanafunzi wa shule yetu wameguswa wameungana na Serikali jana tumekabidhi msaada wetu kwa Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema, "amesema Dewji. 

Dewji ametaja  vitu walivyotoa ni vyandarua, viatu na nguo .
WhatsApp%2BImage%2B2018-05-02%2Bat%2B18.04.26
Kwa upande wake Mjema ameshukuru msaada huo uliotolewa na Shule hiyo.

Sophia Mjema alisema katika wilaya yaIlala nyumba 70 na shule moja zote ziliathirika na mvua za masika. 

"Misaada hii itapelekwa kwa familia zilizopata mafuriko zote  kila mtu itamfikia,"amesema Mjema na kutoa mwito wa kuwataka wananchi wa mabondeni kuondoka mvua kubwa zinakuja hivyo wasikae katika maeneo hatarishi kwa usalama wao.

Wakati huohuo Taasisi ya Khoja Shia Ishanashari Kamat imekabidhidhi msaada wa sinki kwa ajili ya vyoo mia,Taulo za kike na Biskuti. 

No comments:

Post a Comment

APeF Yazindua Mfuko wa Ziada Kupanua wigo wa uwekaji Akiba, Uwekezaji na Ulinzi

  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, (CMSA), CPA Nicodemus Mkama, akikabidhi waraka wa ofa kwa Kaimu Mwenyekiti ...

Pages