Thursday, June 7, 2018
Maendeleo benki imekuza mtaji wake Kwa asilimia 62
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Ibrahim Mwangalaba (kulia), akizungumza na waandishi wa habari katika haflayakutangaza ongezeko la mtaji wa benki hiyo, hafla hiyo imefanyika jana jijini Dar es Salaam kushoto ni Mkuu wa Idara ya fedha wa benki hiyo Peter Tarimo.
Benki ya Maendeleo imeweza kukuza mtaji wake kwa asilimia 62 kutoka bilioni 4.50 mwaka 2013 hadi kufikia bilioni 7.30 sasa.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw.Ibrahim Mwangalaba, jijini Dar es salaam amesema kuwa ongezeko hilo limepatikana Kwa kipindi cha miaka mitano tangu kuanza Kwa benki hiyo.
Pia amefafanua kuwa lengo kubwa la maendeleo benki ni kifikia hadhi ya kuwa benki ya kitaifa na kudumisha utendaji bora wenye tija.
"hadi kufikia mwaka 2017 benki yetu imeweza kupata faida ya milioni 969 na tuna zaidi ya wateja 21,000 haya ni mafanikio makubwa Sana",alisema.
Aidha benki ya Maendeleo imeazimia kufanya mkutano mkuu wa 4 wa mwaka ifikapo Juni 23 mwaka huu kwenye ukumbi wa diamond jubilee jijini humo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...
No comments:
Post a Comment