Tuesday, December 18, 2018
Home
BUSINESS
BENKI YA CBA NA VODACOM YAKABIDHI ZAWADI ZABAJAJI MPYA 5 KWA WASHINDI WA PROMOSHENI YA SHINDA NA M-PAWA
BENKI YA CBA NA VODACOM YAKABIDHI ZAWADI ZABAJAJI MPYA 5 KWA WASHINDI WA PROMOSHENI YA SHINDA NA M-PAWA
Mkurugenzi Idara Wateja binafsi na Masoko wa Benki ya Biashara Afrika (CBA) Julius Konyani (kushoto), akimkabidhi Mshindi wa Bajaji katika promosheni ya Shinda na M-PAWA Bi.Mariam Balawa mkazi wa Kibamba jijini Dar es Salaam, ambapo washindi watano walikabidhiwa bajaji zao na Bi Sophia mkazi wa Bukoba amekabidhiwa kitita cha Shilingi milioni kumi, hafla ya makabidhiano hayo yamefanyika kwenye viwanja vya Benki hiyo Kijitonyama anaeshuhudia (kulia) ni Meneja Masoko wa Vodacom, Noel Mazoya.
Meneja Masoko wa Vodacom, Noel Mazoya (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla yakuwakabidhi washindi wa Bajaji katika promosheni ya Shinda na M-PAWA ambapo washindi watano walikabidhiwa bajaji zao na Bi Sophia mkazi wa Bukoba amekabidhiwa kitita cha Shilingi milioni kumi, hafla ya makabidhiano hayo yamefanyika kwenye viwanja vya Benki hiyo Kijitonyama, (katikati) ni Mkurugenzi Idara Wateja binafsi na Masoko wa Benki ya Biashara Afrika (CBA) Julius Konyani na kulia ni Meneja Biashara Huduma yaM-PAWA Gloria Njiu.
Mkurugenzi Idara Wateja binafsi na Masoko wa Benki ya Biashara Afrika (CBA) Julius Konyani (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla yakuwakabidhi washindi wa Bajaji katika promosheni ya Shinda na M-PAWA ambapo washindi watano walikabidhiwa bajaji zao na Bi Sophia mkazi wa Bukoba amekabidhiwa kitita cha Shilingi milioni kumi, hafla ya makabidhiano hayo yamefanyika kwenye viwanja vya Benki hiyo Kijitonyama, (kushoto) ni Meneja Masoko wa Vodacom, Noel Mazoya na kulia ni Meneja Biashara Huduma ya M-PAWA Gloria Njiu.
Benki ya CBA na Vodacom imekabidhi zawadi kwa washindi wake wa promosheni ya SHINDA NA M-PAWA leo katika tawi la benki hiyo lililopo Kijitonyama.Zawadi hizo ni bajaji tano mpya. Promosheni hiyo iliyodumu wa wiki 6 ilifikia tamati hapo tarehe 14 mwezi huu.
Mshindi wa milioni kumi ni Mama Sophia Sarapion (54) ni mwenyeji wa Bukoba ambapo anaishi akijushughulisha na shughuli ya kilimo cha mihogo, Benki imepanga kumtembelea mshindi huyo mwezi ujao. Washindi watano wa bajaji ambao ni AbeidAbeid, Lucas Ngoye, MariamuBarawa, Hassan MsabilanaHamisiMpela wanatokea maeneo tofauti tofauti ya Tanzania ambayo ni Arusha (1),Chalinze (1) Dar Es Salaam (3).
Mama Sophia ambaye amefurahi sana ameishukuru benki ya CBA na Vodacom kwa kuunda promosheni hii akisema “M-Pawa haijanisaidia tu kwenye maisha yangu ya kila siku linapokuja swala la kutunza akiba na kupata mikopo inayoniwezesha kufanikisha mipango yangu bali imebadilisha maisha yangu kabisa.Nitatumia fedha hizi vizuri katika kuboresha shughuli yangu ya kilimo”
Washindi watano wa bajaji wakiwa wamefurahia sana ushindi huo wameisifia benki ya CBA na Vodacom kwa mkakati wao wa kuirejeshea jamii fadhila kwa njia ya kuwezesha wananchi huku wakiwataka wateja wa M-Pawa kuendelea kutumia M-Pawa na kuwakaribisha ambao bado hawajaanza kutumia kujiunga.
Akizungumza kwenye sherehe hiyo ya makabidhiano ya zawadi hizi kwa washindi,Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa benki ya CBA Bwana Julius Konyani alieleza “Promosheni ya SHINDA NA M-PAWA ililenga kuwafikia wananchi wasiofikiwa na huduma za kibenki na kuwawekea mazingira ya kujiwekea akiba huku ikiwapa changamoto ya kurudisha mikopo yao kwa wakati pale wanapokuwa wamechukua mkopo.Mikopo yetu ina riba ndogo sana kwani lengo letu hasa ni kuwawezesha kiuchumi wateja wetu.Lengo letu jingine ilikuwa kuwashukuru na kuwazawaida wateja wetu msimu huu wa sikukuu.Tunafurahi washindi wetu wameweza kuwa ishara ya mafanikio yetu katika lengo hili
Benki ya CBA kwa ushirikiano na Vodacom tutaendelea kutoa huduma hii ya Mpawa kuweza kuwafikia watanzania wengi zaidi, wakiwemo wakulima na wajasiriamali kuweza kuwakwamua kwa kuwapa mikopo midogo midogo ya mpaka shilingi laki tano. Mbali na hayo M-Pawa inawapa fursa wateja kuhifadhi hela zao kwa malengo yao ya baadae, akiba yako ndio Malengo yako. Katika kipindi hichi cha promosheni tumefanikiwa kuwapata wateja wapya zaidi ya milioni moja wa M-pawa, hivyo Mpawa imekuwa na jumla ya watumiaji wa huduma hii wanayokaribia milioni nane.
Nawapongeza sana washindi wetu wote zaidi ya 1200 na pongezi za kipekee kwa mshindi mkuu na washindi watano waliojishindia bajaji wakawe mabalozi wetu popote watakapopita na waendelee kuhamasisha matumizi ya Mpawa.”
Kampeni ya SHINDA NA M-PAWA ilifanyika kwa muda wa wiki 6 kuanzia tarehe 8 Novemba hadi tarehe 13 Desemba ikilenga watumiaji wa huduma ya M-Pawa.Jumla ya washindi 1,296 walipatikana katika kipindi hicho cha promosheni.Huu ni Ushahidi kwamba jitihada za benki ya CBA na Vodacom katika kuwafikia wananchi wasiofikiwa na huduma za kibenki zinaendelea vyema.
Commercial Bank of Africa (CBA) is a commercial bank in Tanzania, regulated by bank of Tanzania. The bank is a subsidiary of the Commercial Bank of Africa Group.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...
No comments:
Post a Comment