Thursday, December 13, 2018
Watanzania washauriwa kutumia huduma za kibenki za kidijitali
Meneja Masoko na Mawailiano wa Benki ya Barclays Tanzania, Joe Bendera (kushoto), akikabidhi zawadi ya flat screen televisheni ya ukubwa wa inchi 40 kwa mshindi wa kampeni ya’fanya miamala ushinde’ ya benki hiyo, Darius Tebuka, jijini Dar es Salaam jana. Wa pili kutoka kushoto ni maofisa wa Barclays, Theresia Robert na Emmanuel Wangwe
WATANZANIA wametakiwa kutumia mifumo ya kibenki kwa njia za kidigitali badala ya fedha taslimu katika kufanya manunuzi hususani katika msimu huu wa sikukuu ili kujiepusha na vitengo vya wizi na unyang’aji.
Hayo yalisemwa na Meneja Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Barclays Tanzania, Joe Bendera jijini Dar es Salaam jana, wakati wakikabidhi zawadi kwa mshindi wa pili wa kampeni iitwayo ‘fanya miamala ushinde’ inayoendeshwa na benki hiyo.
Kampeni hiyo ya miezi mitatu inahamasidha wateja wa benki hiyo katika kutumia huduma za kidigitali kama vile ATM, na kupitia simu za mkononi ili kufanya malipo mbalimbali kama vile, luku, bili za maji, ving’amuzi, kodi mbalimbali ama kuhamisha fedha kutoka katika akaunti ama kutoka kwenye akaunti kwenda katika mitandano ya simu za mkononi hivyo pia kupunguza muda wa kwenda katika matawi ya benki.
“Natoa hamasa kwa wateja wetu na kwa watanzania kuondokana na tabia ya kutembea na lundo la fedha mfukoni bali watumie huduma za Barclays za njia ya kidigitali kwani ni salama na za uhakika”, alisema.
Katika hafla hiyo, Darius Tebuka alikabidhiwa zawadi ya flat screen television yenye ukubwa inchi 40 aliwashauri watu kutokuwa na wasiwasi na matumizi ya huduma za kibenki kwa njia za kidigitali hapa nchini kwani ni salama na zinasaidia kuwapa muda wa kufanya shughuli nyingine za uzalishaji mali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...
No comments:
Post a Comment