RC MAKONDA AIOMBA TAKUKURU KUCHUNGUZA MIRADI YA DMDP - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Wednesday, April 17, 2019

RC MAKONDA AIOMBA TAKUKURU KUCHUNGUZA MIRADI YA DMDP

 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makinda akiwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke Abdalah Chaurembo (kulia) wakiwa kwenye Ziara Katika Manispaa hiyo ya Ukaguzi maendeleo ya Miradi.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva,  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke Abdalah Chaurembo,  wakimsikiliza DMO Manispaa ya Temeke Dr. Gwamala  Mwabulambo (kulia) akitoa maelekezo ya mradi wa Afya Katika manispaa hiyo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa kukagua miradi mbalimbali.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akizungumza Katika Ziara hiyo


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Paul Makonda amemuagiza Mkurugenzi wa TAKUKURU Mkoa huo kufanya uchunguzi wa utaratibu wa upatikanaji wa tenda kwenye miradi ya DMDP baada ya kubaini matumizi mabaya ya fedha za serikali katika miradi hiyo.

Amesema haiwezekani kuona Kilomita Moja ya Barabara ya DMDP Wilaya ya Kinondoni inajengwa kwa Shilingi Billion 2.7 wakati kwa Wilaya ya Temeke barabara kama hiyo inajengwa kwa shilingi Milioni 900.  

RC Makonda amebaini madudu hayo wakati wa mwendelezo wa ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kupitia fedha zinazotoka Serikali Kuu, Halmashau na pesa za wahisani ambapo amekwazwa na matumizi mabaya ya fedha za mkopo kutoka Bank ya dunia.

Aidha amesema kuwa Barabara  za DMDP zimekuwa zikijengwa kwa kiasi kikubwa cha pesa kuliko zile za TANROAD ambazo kwanza zina ubora mkubwa, uwezo wa kubeba mzigo mkubwa na pia ni Pana.

Katika ziara hiyo  ametembelea miradi ya Ujenzi wa Barabara,Hospital na Shule ambapo ameipongeza Manispaa ya Temeke kwa kusimamia vizuri miradi ya Maendeleo na kuwataka kuongeza kasi.

No comments:

Post a Comment

Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu

Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...

Pages