Thursday, April 18, 2019

RC Makonda aridhishwa na Maendeleo ya Mradi wa Nyumba za Askari Magereza Ukonga.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda,
ikiwa ni katika muendelezo wa ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbli ya
jijini Dar es Salaam, leo ametembelea mradi wa maghorofa 12 ya askari Magereza
unaosimamiwa na Jeshi la Wananchi nchini (JWTZ)uliopo Ukonga jijini hapa.
Ambapo hapo awali ulikuwa unasimamiwa na
Mamlaka ya Ujenzi nchini TBA na Jeshi la Magereza kabla ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kuukabidhi mradi huo kwa JWTZ.
RC
Makonda ameonesha kuridhishwa na maendeleo ya mradi huo na kumpongeza msimazi
wa Uendeshaji ya mradi huo Brigedia Charles Mbuge na mainjinia huku akiwa na
imani kuwa ndani ya miezi miwili na nusu mradi huo utakuwa tayari.
Kwa upande wake Msimamizi Mkuu wa Uendeshaji
ya mradi Brigedia Mbuge ameeleza kuwa katika ghorofa ya chini majengo yote 12
yamefikia asilimia 90% bado asilimia 10% kumaliza kujenga tofali na kuongeza
kuwa ndani ya mud wa wiki moja watakuwa wamemaliza ghorofa ya pili. Ujenzi wa
mradi huo ukikamilika inakadiriwa kuwa familia 172 zitapata makazi huku
maghorofa 8 yakiwa ya askari na manne 4 ya maafisa.
Tags
# LOCAL
Share This
Newer Article
Udhamini wa NBC wang’arisha shindano la Shika Ndinga jijini Dodoma
Older Article
RC MAKONDA AIOMBA TAKUKURU KUCHUNGUZA MIRADI YA DMDP
SERIKALI YATOA MWEZI MMOJA KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE 2024 KUBADILISHA MACHAGUO YA TAHASUSI ZA KIDATO CHA TANO
Hassani MakeroApr 02, 2025Rais Samia ahutubia Baraza la Eid El Fitr Jijini Dar es Salaam
Hassani MakeroMar 31, 2025MWENYEKITI WA CCM MKOA TANGA ASISITIZA AMANI SHEREHE ZA EID ELFITR
Hassani MakeroMar 30, 2025
Labels:
LOCAL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, ikiwa ni katika muendelezo wa ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbli ya jijini Dar es Salaam, leo ametembelea mradi wa maghorofa 12 ya askari Magereza unaosimamiwa na Jeshi la Wananchi nchini (JWT...
No comments:
Post a Comment