Friday, April 12, 2019
Wanafunzi wanaosoma kwa ufadhili wa NBC wanolewa
Mkufunzi kutoka taasisi ya Elevate Education ya Afrika Kusini, Yolisa Motha (kulia) akizungumza na baadhi ya Wanafunzi wa Chuo Uhifadhi Cha Wanyamapori (MWEKA) wanaosoma kwa Ufadhili wa Benki ya NBC wakati wa Mafunzo ya kuwaandaa kimasomo na katika stadi nyingine za kielimu na kimaisha yaliyoandaliwa na benki hiyo, Moshi, Mkoani Moshi hivi karibuni.
Meneja Huduma za Jamii wa NBC, Irene Peter (kushoto) akizungumza na Wanafunzi wa Chuo Cha Uhifadhi Wanyamapori (MWEKA) wanaosoma kwa Ufadhili wa Benki ya NBC wakati wa Mafunzo ya kuwaandaa kufaulu masomo pamoja na ujuzi mwingine wa kimaisha yaliyoandaliwa na benki hiyo Mkoani Moshi, Mkoani Kilimanjaro hivi karibuni.
Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo Cha Uhifadhi Wanyamapori (MWEKA) wakiwa katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa kushirikiana na taasisi ya Elevate Education mjini Moshi hivi karibuni.
Mkuu wa Chuo cha Uhifadhi Wanyama pori, Prof.Jaffari Kideghesho (kulia) akizungumza na Wanafunzi wa Chuo Uhifadhi Cha Wanyamapori (MWEKA) wanaosoma kwa Ufadhili wa Benki ya NBC wakati wa Mafunzo ya kuwaandaa kimasomo na katika stadi nyingine za kielimu na kimaisha yaliyoandaliwa na benki hiyo Moshi, Kilimanjaro hivi karibuni.
Meneja Huduma za Jamii wa NBC, Irene Peter (Wa nne Kushoto, aliyevaa miwani) na Mkufunzi kutoka taasisi ya Elevate Education ya Afrika Kusini, Yolisa Motha (kushoto kwa Irene), wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo cha Uhifadhi Wanyamapori (MWEKA) baada ya mafunzo hayo mjini Moshi, Kilimanjaro hivi karibuni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...
No comments:
Post a Comment