Thursday, October 10, 2019
Home
LOCAL
Benki ya NBC yatoa msaada wa madawa na vifaa tiba kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro
Benki ya NBC yatoa msaada wa madawa na vifaa tiba kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro
Meneja
Uendeshaji wa Benki ya NBC Tawi la Morogoro, Joceline Msuya (wa tatu
kushoto) akizungumza wakati akikabidhi msaada wa madawa na vifaa tiba
vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 9 kusaidia hospitali ya
Rufaa ya
Mkoa wa Morogoro pamoja na nyingine zenye uhitaji vilivyotolewa na NBC
ikiwa ni
sehemu ya shughuli za kuisaidia jamii za benki hiyo zinazoendelea
kufanyika
sehemu mbalimbali nchini. Makabidhiano hayo yalifanyika Hospitalini hapo
Mkoani
Morogoro jana. Kushoto kwake ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya
Rufaa ya
Mkoa wa Morogoro, Dk. Francis Semwene. Hospitali huyo hukabiliwa na
mzigo mkubwa wa kuhudumia wagonjwa wa matukio ya ajali mara kwa mara.
Madawa hayo yamenunuliwa kutoka Bohari Kuu la Madawa Nchini (MSD).
Meneja Uendeshaji wa Benki ya NBC Tawi la Morogoro, Joceline Msuya (wa tatu kulia), akishikana mikono na Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Dk. Francis Semwene wakati akimkabidhi msaada wa Madawa yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 9 kusaidia hospitali hiyo na nyingine zenye uhitaji vilivyotolewa na NBC ikiwa ni sehemu ya shughuli za kuisaidia jamii za benki hiyo zinazoendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini. Makabidhiano hayo yalifanyika Hospitalini hapo Mkoani Morogoro jana. Hospitali hiyo hukabiliwa na mzigo mkubwa wa kuhudumia wagonjwa wa matukio ya ajali mara kwa mara. Madawa hayo yamenunuliwa kutoka Bohari Kuu la Madawa Nchini (MSD).
Meneja Uendeshaji wa Benki ya NBC Tawi Morogoro, Joceline Msuya (wa nne kushoto), akimkabidhi Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Dk. Francis Semwene msaada wa madawa na vifaa tiba vyenye thamani zaidi ya shilingi Milioni 9 kusaidia hospitali hiyo pamoja na nyingine zenye uhitaji vilivyotolewa na NBC ikiwa ni sehemu ya shughuli za kuisaidia jamii za benki hiyo zinazoendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini. Makabidhiano hayo yalifanyika hospitalini hapo, Morogoro jana. Hospitali hiyo hukabiliwa na mzigo wa kuhudumia wagonjwa wa matukio ya ajali mara kwa mara. Madawa hayo yamenunuliwa kutoka Bohari Kuu la Madawa Nchini (MSD).
Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC Tawi la Morogoro, Grace Kapesa (wa nne kushoto), akimkabidhi Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Dk. Francis Semwene msaada wa madawa na vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 9 kusaidia hospitali hiyo pamoja na nyingine zenye uhitaji vilivyotolewa na NBC ikiwa ni sehemu ya shughuli za kuisaidia jamii za benki hiyo zinazoendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini. Hospitali hiyo hukabiliwa na mzigo wa kuhudumia wagonjwa wa matukio ya ajali mara kwa mara. Madawa hayo yamenunuliwa kutoka Bohari Kuu la Madawa Nchini (MSD).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa Tanzania Yakamilisha Kampeni ya Kusisimua ya "Spend & Win" kwa Droo ya Mwisho na Hafla ya Kukabidhi Gari
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Lilian Swere (kushoto), akihutubia hadhira wakati wa droo ya tatu y...
No comments:
Post a Comment