Tuesday, November 5, 2019
Benki ya NBC yaendeleza jitihada zake katika kusaidia huduma za jamii
Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabiashara
Wadogo na wa Kati wa Benki ya NBC, Evance Luhimbo (katikati)
akipokea cheti kutoka kwa Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya Mshindano ya
Gofu ya Hisani yaliyoandaliwa na Klabu ya Rotari ya Bahari, Hemaly Jethwa kwa
kutambua udhamini wa benki hiyo katika mshindani hayo yaliyofanyika katika Viwanja
cha gofu vya Gymkhana jijini Dar es Salaam hivi karibuni yakiwa na lengo la
kukusanya fedha kusaidia wenye mahitaji maaalumu ikiwa ni pamoja na mradi wa
kusaidia upatikanaji wa maji safi na salama, vyoo na kituo cha mafunzo kwa njia
ya mtandao katika Shule ya Sekondari Mtakuja iliyopo Kunduchi jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Meneja Mahusiano wa NBC, Joseph Lema. Mashindano hayo
yaliwashirikisha zaidi ya wacheza gofu 104.
Picha mbalimbali za tukio la
mashindano ya gofu ya hisani yaliyoandaliwa na Klabu ya Rotari ya Bahari na
kudhaminiwa na Benki ya NBC. Mashindano hayo yalikuwa na lengo la kukusanya
fedha na kusaidia wenye mahitaji maaalumu katika jamii ikiwa ni pamoja na mradi
wa kusaidia upatikanaji wa maji safi na salama, vyoo na kituo cha mafunzo kwa
njia ya mtandao katika Shule ya Sekondari Mtakuja iliyopo Kunduchi jijini Dar
es Salaam. Mashindano hayo yaliwashirikiosha zaidi ya wacheza gofu 104.
Maofisa wa Benki ya Taifa ya Biashara
(NBC), wakipiga picha ambapo pamoja na kutoka huduma za maji na kofia kwa
wakimbiaji, washiriki pia walipata nafasi ya kujulishwa huduma mbalimbali za
kibenki zitolewazo na benki hiyo.
Na mwandishi wetu,
KATIKA kuendeleza
jitihada zake za kurudisha sehemu ya faida yake kwa jamii, Benki ya NBC
imedhamini hafla maalumu ya kuchangisha fedha iliyoandaliwa na
Klabu ya Rotari ya Bahari jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Hafla hiyo
iliandaliwa na klabu hiyo ili kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wenye
mahitaji maalumu katika jamii ya watanzania ikiwemo mradi wa kusaidia
upatikanaji wa maji safi na salama, vyoo na ujenzi wa kituo cha kufundishia kwa
njia ya mtandao katika Shule ya Sekondari ya Mtakuja iliyopo eneo la Kunduchi
jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na
gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na wa
Kati wa NBC, Evance Luhimbo alisema NBC kwa miaka kadhaa imekuwa ikishughulisha
katika kusaidia shughuli za jamii katika maeneo mbalimbali kama vile
elimu, afya na masuala ya ujasiriamali,
“Sisi ni jukumu
letu kama benki kurudisha katika jamii sehemu ya faida tuipotayo katika
biashara yetu, NBC ni benki kongwe yenye uzoefu katika kutoa huduma bora za
kibenki kwa zaidi ya miaka 52, hivyo tutaendelea kusapoti miradi kama hii yenye
kuleta tija katika jamii”, alisema.
Pamoja na hayo
alisema mara baada ya kupokea maombi ya kuchangia hafla hiyo kutoka Klabu ya
Rotari, benki yao haikusita kuitikia wito kwani ni imani jamii ikiwezeshwa
kiuchumi na kielimu na jamii ikiwa na afya bora inaweza kuchangia vizuri katika
kuleta maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
Aidha Bwana Lhimbo
aliitaja baadhi ya shughuli za kujamii ambayo NBC imefaya ikiwa ni pamoja
na kutoa vifaa vya ujenzi wa madarasa katika shule za mkoani Lindi,
Zanzibar, msaada wa vifaa tiba katika Hospitali ya Rufaa Morogoro pamoja na
kutoa elimu ya masuala ya kifedha na ujasiriamali katika shule mbalimbali nchini.
Baadhi ya miradi
ambayo imeshafanikishwa na Klabu ya Rotari ya Bahari ni pamoja na matibabu ya
moyo kwa watoto katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), ukarabati wa
maktaba katika shule ya msingi buyuni, upanuzi wa kituo cha mafunzo ya ufundi
stadi katika kituo cha masista cha Carmel, Kurasini, ukarabati wa maktaba
katika Shule ya Sekondari ya Mtakuja pamoja na kutoa misaada ya aina
tofauti katika vituo vingine vya walemavu na wasiojiweza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Biashara DCB kuendelea kuboresha Maisha ya Watanzania
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Bi. Zawadia Nanyaro (wa nne kulia) akishikana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Bias...
No comments:
Post a Comment