MSANII DIAMOND PLATNUMZ NA WASAFI MEDIA WAMUUNGA MKONO RC MAKONDA KAMPENI YA UPASUAJI WA MOYO KWA WATOTO KUTOKA FAMILIA DUNI - THINKING IN BUSINESS

Mgongopr.blogspot.com is a business centered online platform highlighting trade, finance and economic news in Tanzania. Our coverage is customised to ensure we consolidate brands, boost sales and nurture investments. The site is an imprint of Mgongo Logistics and Solutions, a trusted consultancy firm, offering Social Media Management, Photography, Videography, Advertising, Event Management and Translation. For more information contact us via; Phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Tuesday, November 5, 2019

MSANII DIAMOND PLATNUMZ NA WASAFI MEDIA WAMUUNGA MKONO RC MAKONDA KAMPENI YA UPASUAJI WA MOYO KWA WATOTO KUTOKA FAMILIA DUNI


Kampeni ya ufadhili wa matibabu ya Upasuaji wa Moyo kwa Watoto 60 kwa muda wa miezi sita iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda mevuka malengo kutoka Watoto 60 hadi kufikia watoto 90 ikiwa ni ongezeko la watoto 30 jambo linalokwenda kurejesha uhai kwa watoto hao ambao tayari wazazi wao walikuwa wamekata tamaa kutokana na kushindwa kumudu gharama za matibabu.

RC Makonda amesema ongezeko hilo la Watoto 30 limetokana na Kampeni ya uchangishaji wa fedha iliyofanywa na Kituo cha Utangazaji cha Wasafi Media ambao wamefanikiwa kuchangisha kiasi cha Shilingi milioni 60 ambapo kati ya fedha hizo Shilingi Milioni 20 zimetolewa na msanii Diamond na nyingeni zimetolewa na wadau na wasanii mbalimbali wakiwemo Mbosso, Rayvany, Lavalava, Irine Uwoya, Queen Darling, Babutale, Jux, Star Times, DSTV na wadau wengine walioguswa na jambo hilo.

Aidha RC Makonda amemshukuru msanii Diamond kwa kujitolea 20% ya mapato yote yatakayopatikana kupitia tamasha la Wasafi Festival 2019 yatumike kugharamia matibabu ya moyo kwa Watoto waliolazwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

Kwa upande wake Msanii Nasib Abdul almaarufu Kama Diamond Plutnumz amempongeza RC Makonda kwa kuwa kiongozi mwenye Moyo wa Kujali na kubeba changamoto za wananchi anaowaongoza.

No comments:

Post a Comment

ABSA BANK TANZANIA SEES GLOBAL VOLATILITY AS A CATALYST FOR TANZANIAN COMPETITIVE ADVANTAGE

Corporate Banking Director at Absa Bank Tanzania, Ms. Nellyana Mmanyi, addresses participants during a meeting organized for senior business...

Pages