Sunday, November 10, 2019
NBC yazindua Klabu ya Biashara (NBC-B-Club) Mkoani Morogoro
Ofisa
Uvuvi na Mifugo wa Manispaa ya Morogoro, Mohamed Chamzhim (kushoto), aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Morogoro katika uzinduzi wa Klabu ya
Biashara ya Benki ya NBC mkoani Morogoro, akishikana mikono na Mjumbe wa
Bodi ya NBC, Dk. Kassimu Hussein wakati akizindua rasmi klabu hiyo mkoani humo
jana. Kulia ni Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru.
Ofisa
Uvuvi na Mifugo wa Manispaa ya Morogoro, Mohamed Chamzhim (wa tatu kushoto),
aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Morogoro katika uzinduzi wa Klabu ya
Biashara ya Benki ya NBC mkoani humo jana, akishikana mikono na Mjumbe wa Bodi
ya NBC, Dk. Kassimu Hussein katika uzinduzi wa klabu hiyo Mkoani Morogoro
jana. Klabu hiyo imeanzishwa
kusaidia mahitaji ya wafanyabiashara wadogo na wa mkoa huo. Kutoka kushoto
ni Mkurugenzi wa Biashara NBC, Elvis Ndunguru, Mkuu
wa Kitengo cha Wafanyabiashra wa kati na Wadogo, Evance Luhimbo na Meneja wa Tawi la NBC Morogoro, Sophia Mwombelo.
Mkuu
wa Kitengo cha Wafanyabiashra wa Kati na Wadogo wa Benki ya NBC, Evance Luhimbo
akizungumza katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki hiyo kwa
wateja wake wafanyabiashara wadogo na wa kati Mkoani Morogoro jana.
Semina hiyo ilifuatiwa na uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya benki hiyo mkoani
humo.
Ofisa
Uvuvi na Mifugo wa Manispaa ya Morogoro, Mohamed Chamzhim (kushoto), aliyemwakilisha
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro katika uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya Benki ya NBC
mkoani humo akikaribishwa na Mjumbe wa Bodi ya NBC, Dk. Kassimu Hussein wakati
akiwasili kuzindua rasmi klabu hiyo mkoani humo jana. Katikati ni Meneja wa
Tawi la NBC Morogoro, Sophia Mwombelo. Uzinduzi huo ulitanguliwa na
semina ya siku moja juu ya kuwajengea uwezo wafanyabiasha
wadogo na wa kati.
Ofisa
Biashara Mwandamizi Taarifa za Biashara na Takwimu kutoka Mamlaka ya Biashara
Tanzania (Tantrade), Magdalena Shirima akitoa elimu kuhusu fursa za masoko ya
nje ya nchi katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa wateja
wake wafanyabiashara wadogo na wa kati Mkoani Morogoro jana. Semina hiyo
ilifuatiwa na uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya benki hiyo mkoani humo.
Ofisa
Biashara wa Asasi ya Kusaidia Uwekezaji kwenye Kilimo (PASS), Irene
Benedicto akizungumza katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki ya
NBC kwa wateja wake wadogo na wa kati Mkoani Morogoro jana. Semina hiyo
ilifuatiwa na uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya benki hiyo mkoani humo.
Ofisa
Mkuu Msimamizi wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Julius Mjenga
akitoa elimu kuhusu kodi katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki ya
NBC kwa wateja wake wafanyabiashara wadogo na wa kati Mkoani Morogoro jana.
Semina hiyo ilifuatiwa na uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya benki hiyo mkoani
humo.
Baadhi
ya wafanyabiashara wakifuatilia mada katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa wateja wake wafanyuabiashara wadogo na wa
kati Mkoani Morogoro jana. Semina hiyo ilifuatiwa na uzinduzi wa Klabu ya
Biashara ya benki hiyo mkoani humo.
Na mwandishi
wetu, Morogoro
JUHUDI binafsi za wafanyabiashara kwa kushirikiana na taasisi za kifedha
ni moja ya nyenzo muhimu katika kufikia malengo ya mpango mkakati wa serikali
ya awamu ya tano katika kutoa kipaumbele katika uchumi wa viwanda.
Hayo yalisemwa na Mjumbe Mjumbe wa Bodi ya NBC, Dkt. Kassim Hussein katika hafla ya uzinduzi
wa Klabu ya Biashara ya NBC, maarufu kama ‘NBC B-Club’ ya Mkoa wa Morogoro
ikiwa ni klabu ya 11 kuzinduliwa katika mikoa mbalimbali nchini.
“Kwenye biashara serikali imefanya mageuzi makubwa mfano katika kuwahamasisha wafanyabiashara kutumia
mashine za kielektroniki, kurasimishwa kwa biashara, lakini kunahitaji juhudi
kubwa katika kuangalia masuala ya masoko, vifungashio, mitaji na viwango
vya TFDA ili kufanya biashara hizo zikue”, alisema.
Ni kutokana na hayo alisema NBC B-Club itakuwa faida kubwa kwa
wafanyabiashara na nguvu ya kuleta maendeleo kwa taasisi na mtu mmoja mmoja,
huku benki NBC ikiongeza mafunzo ya mara
kwa mara kwa kuleta wataalam mbalimbali na kutoa punguzo la riba kwa wanachama
wa klabu hizo.
Akizungumza zaidi kuhusu klabiu hiyo Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara
NBC, Elvis Ndunguru, alisema lengo pia ni kuwakutanisha wafanyabiashara
mbalimbali ili kuweza kubadilishana uzoefu, kupata fursa mbalimbali za masoko
ndani na nje ya nchi pamoja na kuwaunganisha na wafanyabiashara wa nje.
Ndunguru alisema ni rahisi kutoa nafasi ya elimu kwa wafanyabiashara hao
kupitia klabu zao, kwenye maeneo wanayobaini yanayotakiwa elimu baada ya kupata
mrejesho toka kwa wateja wao.
“Klabu za Biashara tumeshazianzisha maeneo mbalimbali Tanzania, lakini
lengo hasa ni kuwakutanisha wafanyabiashara mbalimbali ili kuweza kugundua
fursa, kuwapa elimu, kuleta wataalam
tofauti, pia kuna fursa za kupeleka wafanyabiashara katika nchi mbalimbali”
alisema Ndunguru.
Pia alisema wanatarajia kuongeza nchi nyingine ambazo zinafanya vizuri
kibiashara ikiwemo Uturuki, Ujerumani na Marekani, na kwamba wana mpango wa
kutengeneza dirisha maalum la wafanyabiashara wanawake wadogo na wakati ili
kuwahamasisha zaidi kuingia katika biashara.
Awali akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Afisa Uvuvi na
Mifugo Manispaa ya Morogoro, Mohamed Chamzimu, alisema Klabu hiyo itawawezesha
wanachama hao kuwa na uelewa wa biashara wa kisasa, na kwamba mafunzo
wanayoyapata yataleta tija na kuongeza weledi katika shughuli zao.
Chamzimu aliwataka wafanyabiashara hao kujitokeza na kujiunga kwa wingi
katika klabu hiyo kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wao Wafanyabiashara hao akiwemo Bupe Kamugisha wameipongeza
benki hiyo kwa huduma bora na masharti nafuu ya kuchukua mikopo, na kusema
kwamba imekuwa haina vitendo vya kutaifisha mali za wateja wao pindi wanapopata
ugumu kwenye marejesho.
Nae mfanyabiashara Lusako Mwakiluma alisema mafunzo waliyoyapata toka
kwa taasisi mbalimbali zikiwemo Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS),
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE),
Shirika la Hifadhi za Jamii (NSSF) yatawasaidia kuboresha biashara zao sambamba
na kujua utaratibu unaowapasa kufuata ili kuweza kukidhi viwango vinavyotakiwa.
Uzinduzi wa klabu hiyo ni wa 11 baada ya Klabu nyingine 10 kuzinduliwa
katika mikoa mingine ikiwemo Mwanza ambayo imeonyesha mafanikio
makubwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Biashara DCB kuendelea kuboresha Maisha ya Watanzania
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Bi. Zawadia Nanyaro (wa nne kulia) akishikana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Bias...
No comments:
Post a Comment