Wednesday, March 4, 2020

Coral Paints yatangaza mafanikio ikitimiza miaka 30
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Insignia Ltd ambao ni
watengenezaji wa Rangi za Coral & Galaxy Paint, Kisan Dhebar (katikati),
akizungumzia maadhimisho ya Miaka 30 ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo
mbele ya waandishi wa habari na wageni wengine waalikwa. Katika hafla hiyo. Katika hafla hiyo kampuni hiyo ilimtangaza msanii Diamond Platnumza kuwa Balozi
mpya wa Coral Paints.
Balozi Mpya wa Rangi za Coral, Msanii wa kizazi kipya Diamond
Platnumz akiimba wimbo, maalum kuhamasisha matumizi ya rangi ya kampuni hiyo
wakati Kampuni ya Insignia Ltd ikimtangaza kuwa balozi sambamba na maadhimisho
ya Miaka 30 ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Insignia Ltd ambao ni
watengenezaji wa Rangi za Coral & Galaxy Paint, Kisan Dhebar (kushoto), na
Balozi Mpya wa Rangi za Coral, Msanii wa kizazi kipya Diamond Platnumz (kushoto
kwake), wakishangilia katika hafla ambayo kampuni hiyo ilitangaza kuadhimisha
miaka 30 tokea kuanzishwa kwake nchini na pia kumtangaza Diamond kama balozi
wao. Wengine ni wawakilishi kutoka Coral Paint na Wasafi Media. Hafla hiyo
ilifayika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Insignia Ltd ambao ni
watengenezaji wa Rangi za Coral & Galaxy Paint, Kisan Dhebar (katikati),
akizungumzia maadhimisho ya Miaka 30 ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo
mbele ya waandishi wa habari. Katika hafla hiyo kampuni hiyo ilimtangaza msanii
Diamond Platnumz kuwa Balozi mpya wa Coral Paints.
Na Mwandishi Wetu,
KAMPUNI ya rangi ya Coral Paints
imeadhimisha miaka 30 tangu ilipoasisiwa huku ikijivunia ushirika wake katika
kukuza uchumi wa wananchi na taifa zima kwa kuwainua mamia ya wajasiliamali
nchini.
Akizungumza wakati wa hafla ya
maadhimisho hayo jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni
hiyo, Kishan Dhebar, alisema wengi miongoni mwa wajasirimali hao kwa sasa ni
mawakala wakubwa wa Coral Paints ndani na nje ya nchi.
“Wapo ambao tulianza nao miaka 30
iliyopita na tumekuwa tukitumia takriban Sh. 100 milioni kila mwaka kwa ajili
ya kuwainua wajasiriamali wa Tanzania. Hadi sasa tuna takriban mawakala 1,500
ndani na nje ya nchi,” alisema Dhebar.
Dhebar alisema Coral Paints katika
miji ya Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma na Moshi ambako ndiko kampuni hiyo
ilikozaliwa mwaka 1990, ikiasisiwa na Watanzania kabla ya kupanuka na kuwa
kinara katika soko la rangi, ikichagizwa na kauli mbiu ya ‘Kupamba na Kusherehekea’.
Akizungumzia mafanikio ya kampuni kwa
miaka yake 30, mmoja wa wafanyakazi, Amani Mosha, alisema iikuwa ni miaka ya
kujivunia kutokana na ubora wa bidhaa wanazozalisha na kuziingiza sokoni.
“Bidhaa zeu ni bora na zenye mng’ao
unaodumu kwa muda mrefu na kukidhi matakwa ya wateja ikionyesha thamani halisi
ya nyumba au garii,” alisema Mosha.
Awali Dhebar alimtambulisha msanii
maarufu nchini, Diamond Platinum kuwa Balozi wa Chapa ya Coral Paints, akisema
kwa kuwa wao huzalisha bidhaa bora, ndio maana wamemchagua mtu bora
kushirikiana nao.
Diamond, kwa upande wake aliahidi
kutoiangusha kampuni hiyo na kwamba atatumia kipaji chake kusambaza ‘simulizi
ya kila ukuta’ kama ilivyo kauli mbiu mpya ya Coral Paints.
“Nitaanza kwanza kwa kuipamba
Tandale. Nyumba ambazo hazijapakwa rangi tutaipaka rangi za Coral ili baadate
tusherehekee,” alisema Diamond.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa ya endelea kusambaza upendo wa Siku ya Wapendanao kwa wajasiriamali
Meneja wa Masuala Endelevu na Matukio wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi, akichagua maua, wakati baadhi ya wafanyakazi wa benki h...

No comments:
Post a Comment