KINONDONI YAPONGEZWA KWA KUJENGA UWANJA WA MPIRA WA KISASA, TIMU KUBWA ZATAKIWA KUIGA MFANO - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Thursday, June 25, 2020

KINONDONI YAPONGEZWA KWA KUJENGA UWANJA WA MPIRA WA KISASA, TIMU KUBWA ZATAKIWA KUIGA MFANO

Naibu Waziri wa Tamisemi Mhe. Josephat Kandege akikagua muonekano wa uwanja wa mpira wa miguu wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni wakati alipotembelea uwanja huo, mwenyesuti ya 'Dark-blue' ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo.

Manispaa ya Kinondoni imepongezwa kwa ujenzi wa uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu wenye uwezo wa kuchukua takriban idadi ya mashabiki 3600 kwa mara moja.

Pongezi hizo zimetolewa na Naibu wa Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Josephat Kandege wakati wa ziara yake katika Halmashauri hiyo kushuhudia uwanja huo wa kisasa ukijengwa katika eneo la Mwenge kwa mapato ya ndani utakaogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 2.2 hadi kukamilika kwake.

Amesema kuwa mradi huo utakapokamilika utawezesha timu ya mpira ya Manispaa hiyo (KMC FC) kupata faida kubwa na hivyo kujiendesha yenyewe kupitia mapato yatakayokusanywa katika uwanja,na kuzitaka timu kubwa ambazo hadi sasa hazina viwanja kuiga mfano huo.

“Niwapongeze sana Kinondoni, kwakujenga uwanja huu, utakapomalizika najua faida yake ipo wazi kabisa, kwanza inapendezesha, lakini pia inaleta changamoto kwa Halmashauri nyingine na timu kubwa kuiga kwenu, kama timu ya Kinondoni inaweza kuwa na uwanja wa kisasa wao wanashindwa nini” amesema Mhe. Kandege.

Hata hivyo Mhe. Kandege ameipongeza timu ya KMC FC kwakuendelea kufanya vizuri katika michezo yake na kusema kuwa kwa mwenendo huo hivi sasa inanafasi kubwa ya kushiriki ligi kuu katika msimu ujao.

No comments:

Post a Comment

Absa Dar City Marathon 2024 zatimua vumbi jijini Dar es Salaam

Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Bwana Aron Luhanga (kushoto), akikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza wa mbio za nu...

Pages