Wednesday, August 26, 2020
Home
LOCAL
DAWASA WAZIDI KUSOGEZA HUDUMA YA MAJI KWENYE MAENEO YALIYOKUWA NA CHANGAMOTO UKOSEFU WA MAJI SAFI
DAWASA WAZIDI KUSOGEZA HUDUMA YA MAJI KWENYE MAENEO YALIYOKUWA NA CHANGAMOTO UKOSEFU WA MAJI SAFI
Mamlaka ya Maji safi na Maji taka Dar es salaam DAWASA katika mkakati wake wa kumtua Mama Ndoo kichwani wameendelea kusogeza huduma ya upatikanaji wa Maji safi na Salama kwa wananchi ambapo kwa sasa wapo katika utekelezaji wa Miradi mikubwa uboreshaji na usambazaji wa kwenye maeneo yenye changamoto ya huduma hiyo.
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka hiyo Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kwa sasa Mamlaka imeamua kuhakikisha 35% ya mapato yake ya ndani yanakwenda kutekeleza ujenzi wa Miradi mikubwa ya kusambaza huduma ya maji kwenye maeneo ambayo hayana Maji.
Aidha Mhandisi Luhemeja amesema miongoni mwa Miradi inayokwenda kumaliza kilio cha Maji Dar es salaam ni pamoja na Ujenzi wa Tank la kupokea Maji kiasi cha lita milioni 14 kutoka visima vya Kimbiji na Mpela kisha kuyasambaza kwenye Maeneo ya Wilaya ya Kiamboni ambapo mradi unatarajiwa kukamikika kabla ya Mwezi April mwakani.
Miradi mingine ni Mradi wa uboreshaji usambazaji wa Maji kutoka Makongo hadi Bagamoyo wenye thamani ya shilingi bilioni 65 na Mradi wa Maji Kisarawe hadi Pugu ambapo ujenzi wa Tank umefikia 70%.
Mhandisi Luhemeja amesema kwa sasa hali ya upatikanaji wa Maji safi Jijini Dar es salaam imefikia 88% na lengo la Mamlaka hiyo ni kuhakikisha huduma inawafikia watu wote.
Pamoja na hayo Mhandisi Luhemeja amesema katika kipindi cha miaka mitano Makusanyo yamepanda kutoka Shilingi Bilioni 2 mwaka 2015 hadi kufikia Bilioni 12.3 ambapo katika mwaka wa fedha 2020-2021 wamedhamiria kufikia Bilioni 17.
Hata hiyo Mhandisi Luhemeja amemshukuru Rais Dkt. John Magufuli kwa maboresho makubwa aliyofanya kwenye sekta ya Maji huku akiendelea kuwasisitiza wananchi kulipa bili za Maji kwa wakati.
#Dawasa_tunatekeleza_kwa_vitendo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...
No comments:
Post a Comment