RC KUNENGE AMTAKA MKANDARASI WA KAMPUNI YA NYANZA KUKAMILISHA UJENZI WA DARAJA LA KIVULE KABLA YA SEPTEMBER 30 - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Tuesday, August 18, 2020

RC KUNENGE AMTAKA MKANDARASI WA KAMPUNI YA NYANZA KUKAMILISHA UJENZI WA DARAJA LA KIVULE KABLA YA SEPTEMBER 30

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge akiongea na waandishi wa habari, mara baada ya kufanya ukaguzi wa ujenzi wa Daraja linalojengwa na Kampuni ya Nyanza lililopo katika barabara Kitunda-Kivule eneo la Mwailafu.

Muonekano wa Daraja linalojengwa na Kampuni ya Nyanza katika barabara itokayo Kitunda kuelekea Kivule.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amemuelekeza Mkandarasi wa Kampuni ya Nyanza inayojenga barabara na Daraja la Kivule kuhakikisha ifikapo September 30 daraja hilo linakamilika na kuanza kutumika ili kupunguza kero ya usafiri kwa wananchi.

RC Kunenge ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya Ujenzi wa miundombinu Wilaya ya Ilala na Temeke ambapo ameonyesha kuridhishwa na hatua ya ujenzi ilipofikia na kuwataka waongeze juhudi.

Aidha RC Kunenge amesema ujenzi wa Madaraja hayo unaenda sambamba na ujenzi wa Barabara ya Kuelekea Hospital ya Wilaya ya Ilala iliyopo Kivule ambapo amewasisitiza TANROAD na TARURA kusimamia vizuri miradi hiyo na kuhakikisha inakamilika kwa wakati.


Akiwa kwenye ukaguzi wa Barabara ya Mbosi RC Kunenge amemuelekeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke kuhakikisha anatoa fedha za kumalizia ujenzi wa Barabara hiyo ili ikamilike ndani ya mwezi mmoja.

Pamoja na hayo RC Kunenge amesema tayari amewaelekeza Wakuu wa Wilaya za Mkoa huo kuhakikisha wanatoka maofisini na kwenda kusikiliza kero za wananchi pamoja ukaguzi wa miradi ya maendeleo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge akitoa maelekezo mara baada ya kufanya ukaguzi wa ujenzi wa Daraja linalojengwa na Kampuni ya Nyanza lililopo katika barabara Kitunda-Kivule eneo la Mwailafu.

No comments:

Post a Comment

Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu

Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...

Pages