TANZANIA YASHIRIKI UFUNGUZI WA MTAA WA KUUZA KAHAWA KUTOKA AFRIKA, JIMBO LA HUNAN, CHINA - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Wednesday, August 19, 2020

TANZANIA YASHIRIKI UFUNGUZI WA MTAA WA KUUZA KAHAWA KUTOKA AFRIKA, JIMBO LA HUNAN, CHINA


Hafla ya ufunguzi wa Mtaa wa Kahawa ilifuatiwa  na Mkutano wa biashara uliohudhuriwa na washiriki 360 (onsite) na 2000 (online) ambapo nchi za Tanzania, Ghana na Ethiopia zilipata fursa ya kuwasilisha mada juu ya fursa za biashara ya mazao ya kilimo na uwekezaji katika viwanda.

Hunan Galquiao Grand Market ni soko la (3) kwa ukubwa nchini China linalouza bidhaa mbalimbali kutoka ndani na nje ya China. Uzinduzi wa Mtaa wa Kuuza Kahawa kutoka Afrika ni sehemu ya hatua za Jimbo la Hunan kufungua soko lake kwa bidhaa kutoka barani Afrika.


Katika hafla hiyo ya uzinduzi wa Mtaa wa Kahawa Mabalozi walipata fursa ya kutembelea migahawa inayouza kahawa kutoka Nchi za Tanzania, Ethiopia; Kenya na Rwanda. Vilevile, Mabalozi walipata fursa ya kukutana na Makampuni yanayonunua kahawa (whole sale buyers)

Balozi wa Tanzania Ndugu Mbelwa Kairuki aliyakaribisha makampuni ya Jimbo la Hunan kuwekeza nchini Tanzania kwa kujenga viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo yanayolimwa Tanzania ikiwa ni pamoja na Korosho, Pamba, Katani, Ufuta, Muhogo, Karanga na Soya.

Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki (wa pili kulia) akipatiwa maelezo na mmoja wa wataamu wa Kahawa wakati hafla ya ufunguzi wa Mtaa wa Kahawa, iliyofanyika hivi karibuni katika Jimbo la Hunan.
Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki akihutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mtaa wa Kahawa, iliyofanyika hivi karibuni katika Jimbo la Hunan.

No comments:

Post a Comment

Benki ya Biashara DCB kuendelea kuboresha Maisha ya Watanzania

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Bi. Zawadia Nanyaro (wa nne kulia) akishikana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Bias...

Pages