Benki ya DCB yaendelea kutoa fursa za maendeleo kwa Vicoba - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Friday, September 4, 2020

Benki ya DCB yaendelea kutoa fursa za maendeleo kwa Vicoba

Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya Biashara ya DCB, Zacharia Kapama (wa pili kushoto), akizungumza wakati wa uzinduzi wa miradi ya maendeleo ya asasi isiyo ya kiserikali inayotoa usimamizi na uangalizi wa Vicoba (UYACODE), uliofanyika pamoja na utambulisho wa benki hiyo kama mdau wao muhimu wa maendeleo baada kuingia makubaliano ya ushirikiano. Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya asasi hiyo, Dar es Salaam jana. Wengine kutoka kushoto ni, Meneja wa Tawi la DCB Mabibo, Dorah Kalinga, Mkurugenzi Mtendaji wa Uyacode, Michael Mgawe na Mwenyekiti wa Bodi ya asasi hiyo, Agnes Mangula.
Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya Biashara ya DCB, Zacharia Kapama (wa pili kushoto), na wengine kutoka kushoto; Meneja wa Tawi la DCB Mabibo, Dorah Kalinga, Mkurugenzi Mtendaji wa asasi isiyo ya kiserikali inayotoa usimamizi na uangalizi wa Vicoba (UYACODE), Michael Mgawe, na Mwenyekiti wa Bodi ya asasi hiyo, Agnes Mangula, wakishangilia muda mfupi baada ya uzinduzi wa miradi ya maendeleo ya asasi isiyo ya kiserikali inayotoa usimamizi na uangalizi wa Vicoba (UYACODE), uliofanyika pamoja na utambulisho wa benki hiyo kama mdau wao muhimu wa maendeleo baada kuingia makubaliano ya ushirikiano. Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya asasi hiyo, Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya Biashara ya DCB, Zacharia Kapama, akihojiwa na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa miradi ya maendeleo ya asasi isiyo ya kiserikali inayotoa usimamizi na uangalizi wa Vicoba (UYACODE), uliofanyika pamoja na utambulisho wa benki hiyo kama mdau wao muhimu wa maendeleo baada kuingia makubaliano ya ushirikiano. Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya asasi hiyo, Dar es Salaam jana.
MkurugenzI Mtendaji wa asasi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na usimamizi na uangalizi wa Vicoba (UYACODE), Michael Mgawe (kulia), akikabidhi nakala ya jarida la taasisi hiyo kwa Mkurugenzi wa Biashara wa DCB, Zacharia Kapama katika hafla ya uzinduzi wa miradi ya maendeleo ya asasi hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Tawi la DCB Mabibo.
Baadhi ya wafanyakazi wa DCB wakifuatilia uzinduzi wa miradi ya maeneleo ya asasi ya Uyacode jana makao makuu ya asasi hiyo, Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu

Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...

Pages