Wednesday, October 28, 2020

Marekani yataka Armenia na Azerbaijan kukumbatia Diplomasia
Na Patrick Nduwimana | Washington DC | Waziri wa mambo ya nje wa marekani Mike Pompeo amezisihi Armenia na Azerbaijan kufikia suluhisho la kidiplomasiya kuhusu mzozo kati yao wa kudhibiti jimbo lenye ugomvi la Nagorno Karabakh, ambako ghasia zilizoanza miezi miwili iliopita ziliendelea jana jumanne, licha ya mkataba wa kusitisha mapigano uliofikiwa na pande zote mjini Washington.
Akiwa ziarani nchini India, Pompeo alizungumza kwa njia ya simu na waziri mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan pamoja na rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev.
Pompeo amewashinikiza viongozi hao wawili kutekeleza ahadi zao za kusitisha mapambano na kutafuta suluhisho la kidiplomasiya, taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya marekani imesema.
Jumanne, nchi mbili kila mmoja imeishtumu nyingine kushambulia ngome zilizoko nje ya Nagorno Karabakh, baada ya mkataba wa sitisho la mapigano uliopatikana kutokana na juhudi za waziri Pompeo.
Tags
# INTERNATIONAL
Share This
Newer Article
Absa Bank Tanzania empowers its SME customers with financial literacy in Dar.
Older Article
TWIGA A TRIUMPH OF PARTNERSHIP
Light Upon Light Summit in Zanzibar Set to Inspire and Unite Global Muslim Community12th & 13th October 2024.
kilole mzeeSept 30, 2024MAKAMU WA RAIS AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS KAGAME
Hassani MakeroSept 07, 2022KATIBU MKUU DKT. ALLAN KIJAZI AFANYA ZIARA FUPI EXPO 2020 DUBAI
Hassani MakeroNov 28, 2021
Labels:
INTERNATIONAL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Na Patrick Nduwimana | Washington DC | Waziri wa mambo ya nje wa marekani Mike Pompeo amezisihi Armenia na Azerbaijan kufikia suluhisho la kidiplomasiya kuhusu mzozo kati yao wa kudhibiti jimbo lenye ugomvi la Nagorno Karabakh, ambako ghasia zilizo...
No comments:
Post a Comment