Benki ya Absa yatoa msaada wa vifaa vya usafi kwa shule za Dodoma - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Monday, February 1, 2021

Benki ya Absa yatoa msaada wa vifaa vya usafi kwa shule za Dodoma

Mwakilishi wa Benki ya Absa tawi la Dodoma, Elizabeth Kiwale (wa pili kushoto), akimkabidhi vifaa vya usafi ndoo na sabuni Mwalimu  Mkuu wa Shule ya Msingi Ipagala B, Plaxeda Fundisha, ( wa tatu kulia) katika hafla ya uzinduzi wa ugawaji vifaa vya usafi kwa shule za msingi 54 ulioratibiwa na Shirika la Pact Tanzania kupitia mradi wa WASH unaodhaminiwa na Absa. Uzinduzi huo ulifanyika jana shuleni hapo, jijiji Dodoma. Wa tatu kushoto ni mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa, Mazengo Eliasi na kushoto ni Beatrice Kamugisha kutoka Pact Tanzania.

Mwakilishi  wa Benki ya Absa Tanzania, Elizabeth Kiwale akizungumza na walimu, wanafunzi, na wadau mbalimbali katika hafla ya uzinduzi wa ugawaji vifaa vya usafi kwa shule za msingi 54 vilivyotolewa kwa udhamini wa Absa, jana katika Shule Msingi Ipagala B jijini Dodoma
Wawakilishi kutoka benki ya Absa Tanzania,  Elizabeth Kiwale na Happy Alipipi pamoja na wahudhuriaji wengine wakinawa mikono kwa kutumia vifaa vilivyotolewa msaada na benki hiyo katika hafla ya ugawaji wa vifaa hivyo  kwa Shule ya Msingi Ipagala B, jijini Dodoma.
Mwanafunzi wa Shule ya Ipagala B, Jesca Saimon pamoja na mwenzake wakinawa mikono baada kukabidhiwa  vifaa vya usafi kutoka Benki ya Absa shuleni kwao, Dodoma jana.

No comments:

Post a Comment

Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu

Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...

Pages