Tuesday, October 5, 2021
Home
BUSINESS
BENKI YA BIASHARA YA DCB YADHAMINI KONGAMANO LA 5 LA BARAZA LA TAIFA LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI (NEEC)
BENKI YA BIASHARA YA DCB YADHAMINI KONGAMANO LA 5 LA BARAZA LA TAIFA LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI (NEEC)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) akikabidhi cheti cha shukurani ya udhamini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa wakati wa kongamano la tano la uwezeshaji lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lenye kauli mbiu ya uwezeshaji kwa uchumi jumuishi lililofanyika jijini Dodoma jana. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka na Waziri wa Uwekezaji, Geoffrey Mwambe.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Queen Sendiga (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (wa pili kulia) wakati wa kongamano la tano la uwezeshaji lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) lenye kauli mbiu ya uwezeshaji kwa uchumi jumuishi lililofanyika jijini Dodoma jana. Kutoka kushoto ni Meneja wa Tawi la DCB Dodoma, Daniel Buzuka, Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma, Steven Ndaki na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Generali Wilbert Ibuge. DCB ilikuwa moja ya wadhamini wa kongamano hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Geofrey Ndalahwa (wa pili kushoto) akichangia mjadala wakati wa kongamano la tano la uwezeshaji lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) lenye kauli mbiu ya uwezeshaji kwa uchumi jumuishi lilifanyika jijini Dodoma Jana. DCB ilikuwa moja ya wadhamini wa kongamano hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Geofrey Ndalahwa (katikati) akipozi kwa picha ya kumbukumbu na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo tawi la Dodoma wakati mkurugenzi huyo alipokwenda jijini humo kuhudhuri kongamano la tano la uwezeshaji lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) lenye kauli mbiu ya uwezeshaji kwa uchumi jumuishi. DCB ilikuwa moja ya wadhamini wa kongamano hilo.
Meneja wa Benki ya Biashara ya DCB Tawi la Dodoma, Daniel Buzuka (kushoto), akihudhuria pamoja na wengine, kongamano la tano la uwezeshaji lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) jijini Dodoma jana, lenye kauli mbiu ya uwezeshaji kwa uchumi jumuishi ambalo DCB ilikuwa ni moja ya wadhamini wa kongamano hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Martine Shigella (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Godfrey Ndalahwa wakati wa kongamano la tano la uwezeshaji lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) lenye kauli mbiu ya uwezeshaji kwa uchumi jumuishi. DCB ilikuwa moja ya wadhamini wa kongamano hilo lililofanyika jijini Dodoma jana. Wa pili kushoto ni, Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma, Steven Ndaki na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Generali Wilbert Ibuge.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...
No comments:
Post a Comment