NIC Yaingia Makubaliano Ya Mkataba Wa Udhamini Wa UDSM Marathon - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Tuesday, November 30, 2021

NIC Yaingia Makubaliano Ya Mkataba Wa Udhamini Wa UDSM Marathon

 
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa NIC Yassaya Mwakifulefule (kushoto) na Mkurugenzi UDSM Marathon Dk.Lulu Kaaya wakibadilishana hati za Makubaliano kwa ajili ya UDSM marathon.
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa NIC Yassaya Mwakifulefule (kushoto) na Mkurugenzi UDSM Marathon Dk.Lulu Kaaya wakionesha hati za makubaliano mara baada ya kuzisaini.
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa NIC Yassaya Mwakifulefule (kushoto) na Mkurugenzi UDSM Marathon Dk.Lulu Kaaya wakisaini Makubaliano ya NIC kudhamini mbio.
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa NIC Yassaya Mwakifulefule akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini Makubaliano ya Udhamini UDSM marathon.
  • Dk.Jakaya Kikwete mgeni rasmi wa mbio
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam | RAIS Mstaafu wa awamu ya Nne na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk. Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi wa UDSM Marathon zitazofanyika Desemba 4 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Mbio hizo zimeingiwa na Makubaliano wa Mkataba wa Udhamibi ya Shirika la Bima la Taifa (NIC) na UDSM Marathon ambapo NIC imekuwa mdau mhimu kwa Chuo Kikuu kikongwe katika kwenda bega kwa bega.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja (NIC) Yessaya Mwakifulefule amesema wamekuwa wakitoa mchango mkubwa katika sekta ya michezo kwa lengo la kukuza vipaji kwa watanzania na pia katika kujenga afya ya kujiepusha na magonjwa yasiyoambukiza.

Amesema wana kila sababu ya kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa maana wamekuwa wadau wakubwa kwao katika biashara pia ndio Chuo Kikongwe nchini na kina mchango mkubwa kwa watendaji wa shirika kwa kusoma chuo hicho.

"Ni mara yetu ya kwanza kuipiga jeki UDSM Marathon na haitakuwa mara ya mwisho kufanya hivyo, tutaendelea kushirikiana kama ambavyo wamekuwa wadau wakubwa kwetu kwa muda mrefu tangu shirika lilivyoanzishwa". Amesema Bw.Mwakifulefule.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa UDSM Marathon Lulu Kaaya amesema katika mbio hizo wanatarajia kuwepo k mgeni rasmi Dkt.Jakaya Kikwete pia atashiriki kukimbia Kilomita 5.

Amesema mbio hizo zitakuwa na ruti kubwa tatu ambazo ni ruti ya Kilomita 21.ruti ya kilomita 10 na ruti pamoja na kilomita 5.

'Lengo kuu la mbio hizi ni kwa ajili ya uchangishaji wa fedha kwaajili ya kuboresha maisha ya wanachuo. Kwasasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kipo katika ujenzi wa kituo cha wanafunzi (Student Center) inayojengwa kwenye Campus ya Mwalimu Nyerere Mlimani Jijini Dar es Salaam ambacho ni mahususi kwa kutoa mazingir mazuri ya mapumziko kwa wanafunzi". Amesema

No comments:

Post a Comment

Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu

Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...

Pages