Sunday, November 28, 2021

RC MONGELA AWATAKA VIONGOZI KUSIMAMIA MIRADI YA MAJI ARUSHA
Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela akizungumza na wadau wa maji jijini Arusha kulia kwake ni Bi Valentina Masanja ambaye ni msimamizi wa watoa huduma za maji kutoka wizara ya Maji. (Picha na Jane Edward, Arusha)
Mkuu wa wilaya ya Longido Nurdin Babu akizungumzia changamoto ya maji katika wilaya yake wakati wa mkutano huo.
Na Jane Edward, Arusha | MKUU wa Mkoa wa Arusha John Mongela amewataka wenyeviti, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wote kusimamia miradi ya maji ili kuweza kuondoa Changamoto ya upatikanaji maji katika Mkoa wa Arusha.
Mongela ameyasema hayo katika mkutano wa watoa huduma ya maji ngazi ya jamii (CBWSOs)na wadau wa sekta ya maji vijijini mkoani Arusha.
Amesema lengo la serikali ya Mama Samia ni kuhakikisha miradi ya maji inakamilika kwa haraka ili wananchi waweze kupata maji kwa uhakika.
Amebainisha vipo vifaa vya kutengenezea miundombinu ya maji vinacheleweshwa na hivyo kukwamisha utekelezaji wa miradi ya maji kwa wakati ambapo ameomba wizara ya maji kuwahisha vifaa hivyo ili kutokwamisha miradi hiyo.
"RUWASA mna kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha maji yanapatikana,mimi nataka wilaya za Mkoa wa Arusha ziwe kwenye hali nzuri ya upatikanaji maji,kwahiyo tushirikiane kwenye hili"amesema Mongela.
Kwa upande wake Meneja wa watoa huduma za maji ngazi ya jamii nchini Valentina Masanja anasema anatambua kuwa maji ni siasa na siasa hiyo ipigwe kwa uwangalifu ili maji yaweze kupatikana kwa haraka ingawa ruwasa ilipotoka na ilipo sasa imepiga hatua kubwa sana.
Amesema wanasiasa wasaidie kuhakikisha kuwa wananchi wanatoa ushirikiano katika upatikanaji maji kwani haki inaenda sambamba na wajibu.
Hata hivyo amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa maelekezo aliyoyatoa wao kama wizara watayafanyia kazi ili kuhakikisha malengo ya serikali katika sekta ya maji yanakamilika.
Tags
# LOCAL
Share This
SERIKALI YATOA MWEZI MMOJA KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE 2024 KUBADILISHA MACHAGUO YA TAHASUSI ZA KIDATO CHA TANO
Hassani MakeroApr 02, 2025Rais Samia ahutubia Baraza la Eid El Fitr Jijini Dar es Salaam
Hassani MakeroMar 31, 2025MWENYEKITI WA CCM MKOA TANGA ASISITIZA AMANI SHEREHE ZA EID ELFITR
Hassani MakeroMar 30, 2025
Labels:
LOCAL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela akizungumza na wadau wa maji jijini Arusha kulia kwake ni Bi Valentina Masanja ambaye ni msimamizi wa watoa huduma za maji kutoka wizara ya Maji. (Picha na Jane Edward, Arusha)Mkuu wa wilaya ya Longido Nurdin Ba...
No comments:
Post a Comment