Monday, January 31, 2022
Huawei Yashika Nafasi Ya Juu Tuzo Za Mwajiri Bora
Mkurugenzi Mwajiri wa Huawei wa eneo la kusini mwa Afrika Bw. Chen Yu.
Kampuni ya kimataifa ya mawasiliano Huawei imeshika nafasi ya juu katika tuzo za mwajiri bora wa mwaka.
Huawei imefanikiwa kutwaa cheti maalum ya mwajiri bora katika eneo la jangwa la Sahara baada ya kushindanishwa katika nchi 9 ambazo ni Afrika kusini, Zambia, Kenya, Nigeria, Angola, Ghana, Botswana, Mauritius and Uganda.
Top Employer Institute ni tuzo/cheti maalum zinazotolewa na mamlaka inayosimamia ubora wa utendaji wa watu katika eneo la kazi ambapo tuzo zake huandaliwa kwa kushirikisha makampuni mbalimbali kwa kupimwa kuitia vigezo na masharti mbalimbali na baadaye kupata washindi.
Tuzo hiyo imeelezea kuwa pamoja na hali ya kazi na biashara kuwa mbaya katika makampuni na taasisi mbalimbali kutokana na kuingia kwa virusi vya UVIKO 19 Huawei imefanikiwa kuhakikisha wafanya kazi wake wanabaki salama katika ukanda huo.
Katika kipindi chote cha Uviko 19, Huawei imekuwa ikihakikisha kuwa wafanya kazi wake wanapewa nafasi ya juu ya upendeleo hali iliopelekea huduma yake ya kimtandao kuendelea vizuri na kuipa Huawei nafasi ya kuwa chaguo la mwajiri bora. “Haya ni mafanikio makubwa na ya kuigwa kwa Huawei Afrika kuendelea kutambuliwa kwenye ubora katika eneo hili” alisema Mkurugenzi Mwajiri wa Huawei wa eneo la kusini mwa Afrika Bw. Chen Yu.
“Kama taasisi tunatambua kuwa mtaji wa maarifa bora ya kazi tulionao ndio thamana kubwa, na kwamba tutaendelea kuhakikisha kuwa tunatoa huduma bora kwa watu wetu bila kuyumba” aliongeza Bw. Yu.
Akizungumzia tukio hilo, kiongozi program ya Top Employer Institute Bw. David Plink amesema kuwa miaka miwili iliyopita imeyumbisha sana makampuni na taasisi mbalimbali duniani lakini Huawei imeendeleea kuwa imara hasa katika kuhakikisha kuwa utendaji kazi kwa wafanyakazi wake unaimarika vizuri.
Tuzo za Mwajiri bora wa mwaka zizilizoanzishwa miaka 30 iliyopita zimeshatolewa kwa taasisi Zaidi ya 1857 katika nchi 123 ambapo taasisi zilizopata tuzo hizo ziliweza kugusa Maisha ya wafanya kazi Zaidi ya milioni na duniani. Tuzo za mwajiri bora hutolewa kwa taasisi zinazofanikiwa kufikia vigezo na masharti iliyowekwa ambazo ni rasilimali bora na mazingira bora ya ufanyaji kazi, uwezo, mafanikio, elimu na afya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...
No comments:
Post a Comment