Tuesday, March 1, 2022
Wafanyakazi wa Absa Tanzania wajitolea damu kusaidia wodi ya wazazi ya CCBRT
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Hellen Siria (kushoto) akijitolea damu katika zoezi lililoandaliwa na wafanyakazi wa benki hiyo kutoa damu kwa ajili ya kusaidia wodi mpya ya wazazi katika hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kutoka kulia ni Muuguzi Mkunga wa hospitali ya CCBRT, Emiliana Tibilikirwa na Fundi Sanifu wa Maabara ya Hospitali hiyo, Athumani Daffa.
Meneja Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania, Linda Lance (kulia) akipata vipimo kabla ya kujitolea damu katika zoezi lililoandaliwa na wafanyakazi wa benki hiyo kutoa damu kwa ajili ya kusaidia wodi mpya ya wazazi katika hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Wanaomhudumia kutoka kushoto ni Afisa Muuguzi wa Hospitali ya CCBRT, Christina Baluhya na Fundi Sanifu wa Maabara ya Hospitali hiyo, Athumani Daffa.
Product Implementation Analyst, Ridhiwan Ibrahim (kulia) na Meneja Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania, Linda Lance (wa pili kulia) wakijitolea damu katika zoezi lililoandaliwa na wafanyakazi wa benki hiyo kutoa damu kwa ajili ya kusaidia wodi mpya ya wazazi katika hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam hivi karibuni. kutoka kushoto ni Afisa Muuguzi wa Hospitali ya CCBRT, Christina Baluhya na Fundi Sanifu wa Maabara ya Hospitali hiyo, Athumani Daffa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...
No comments:
Post a Comment