- Airtel Tanzania miongoni mwa himaya tatu za Airtel zitakazohamia teknolojia ya 5G hivi karibuni
Thursday, June 22, 2023
Home
BUSINESS
Airtel Afrika yaitaja Tanzania Miongoni mwa nchi Tatu kuwashwa Masafa ya Teknolojia ya Mawasiliano ya kasi ya 5G
Airtel Afrika yaitaja Tanzania Miongoni mwa nchi Tatu kuwashwa Masafa ya Teknolojia ya Mawasiliano ya kasi ya 5G
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Airtel Africa, kampuni inayoongoza katika kutoa huduma za mawasiliano na za kuhamisha pesa kwa kutumia simu za mkononi, ikiwa imejikita katika nchi 14 barani Afrika, leo hii nchini Nigeria imezindua mchakato wa kuhamia masafa ya mtandao wa 5G ili kutoa huduma za kisasa na kasi Zaidi kwa wateja wake wote huku ikibainisha Tanzania itafuta kuwashwa kwa teknolojia hiyo ya mawasiliano ya kisasa ya 5G.
Uzinduzi wa masafa hayo ya mtandao wa 5G utafanyika awali katika nchi tatu ikianza Nigeria, ikifuatiwa na Tanzania na Zambia, huku mipango ikiwa inaandaliwa ya kusambaza maeneo yaliyobaki kwenye soko zima.
Kwa kutumia 5G, wateja sasa wanaweza kufurahia kuangalia video zikiwa ngáavu zaidi ya ilivyo sasa, kufurafia kutazama michezo mtandaoni, kurusha matukio mubashara Pamoja na kufurahia kasi zaidi wakiwa popote. Kutokana na kwamba wigo wa mawasiliano utapanuka zaidi kutokana na teknolojia ya kisasa ya 5G pia shughuli za biashara zitaimarika hasa zile zinazotumia mtandao kutoa huduma zake, pamoja na kufanikisha mikutano ya mbali mubashara kupitia mtandao.
Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Airtel Afrika Group, Segun Ogunsanya alisema: “Kupitia mtandao wa 5G, tunawapa wateja wetu fursa ya kuishi kidijitali kwa kufurahia maajabu yanayoweza kufanywa na mtandao huu wa teknolojia ya mawasiliano ya kisasa ya 5G. Kwa kukamilisha hili kwa nchi zetu hizi tatu Ikiwemo Tanzania tunadhihirisha tunadhihirisha dhamira yetu tuliyojiwekea ya kuwekeza katika teknolojia ya mtandaoni ya kisasa zaidi ili kufungua wigo mpana na kutoa fursa kwa watumiaji kufanya makubwa, tunawezesha kuiunganisha dunia kidijitali pamoja na wateja wetu kukamilisha maono waliyonayo.”
Mtandao wa 5G utajikita zaidi katika maeneo maalum, mfano maeneo ya makazi yenye msongamano mkubwa wa watu na yale yenye huduma kama maduka, hospitali, maeneo ya kati ya mji na maeneo makuu ya kibiashara na mjini. Wakiwa katika maeneo haya mahsusi ya 5G ambayo yatatambulika rasmi na kuwekewa alama, wateja wanaweza kufurahia mtandao kwa kasi ya mara kumi zaidi ya kawaida, na kurusha picha za video za ubora wa hali juu mubashara bila ya kukatika katika. Mtandao wa 5G unaweza kuunganishwa tu kupitia vifaa vinavyoendana nao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...
No comments:
Post a Comment