Tuesday, August 1, 2023
Home
BUSINESS
Benki ya Absa Tanzania kuziwezesha biashara ndogo na za kati kupitia mikopo yenye dhamana kutoka Mfuko wa Dhamana Afrika (AGF)
Benki ya Absa Tanzania kuziwezesha biashara ndogo na za kati kupitia mikopo yenye dhamana kutoka Mfuko wa Dhamana Afrika (AGF)
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bwana Obedi Laiser (wa pili kushoto), akizungumza jijini Dar es Salaam leo, katika hafla ya utiaji saini makubaliano na Mfuko wa Dhamana Afrika (AGF), ambapo kupitia makubaliano hayo Absa itatoa mikopo maalumu kwa dhamana kutoka mfuko huo. Mikopo hiyo itawalenga wafanyabiashara wadogo na wa kati. Kutoka kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la AGF, Bwana Jules Ngankam, Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Absa, Bwana Melvin Saprapasen Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Absa Tanzania, Bwana Aron Luhanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bwana Obedi Laiser (kulia), na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Dhamana Afrika (AGF), Bwana Jules Ngankam wakitia saini hati za makubaliano yatakayoiwezesha Benki ya Absa kutoa mikopo kwa dhamana kutoka mfuko huo. Mikopo hiyo itawalenga wafanyabiashara wadogo na wa kati hususan wanawake na vijana. Wanaoshuhudia ni maofisa kutoka AGF na Absa. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bwana Obedi Laiser (kulia), na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Dhamana Afrika (AGF), Bwana Jules Ngankam wakibadilishana hati za makubaliano yatakayoiwezesha Benki ya Absa kutoa mikopo kwa dhamana kutoka mfuko huo. Mikopo hiyo itawalenga wafanyabiashara wadogo na wa kati hususan wanawake na vijana. Wanaoshuhudia ni maofisa kutoka AGF na Absa. Ilikuwa ni katika hafla ya utiaji saini makubaliano hayo jijini Dar es Salaam leo. Wanaoshuhudia ni maofisa kutoka Absa na AGF.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara, Bwana Melvin Saprapasen (wa pili kulia), akizungumza katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bwana Obedi Laiser (wanne kushoto), na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Dhamana Afrika (AGF), Bwana Jules Ngankam (wa tatu kushoto), wakipiga picha ya kumbumbuku muda mfupi baada ya kutia saini makubaliano yatakayoiwezesha Benki ya Absa kutoa mikopo kwa dhamana kutoka mfuko huo. Mikopo hiyo itawalenga wafanyabiashara wadogo na wa kati hususan wanawake na vijana. Wanaoshuhudia ni maofisa kutoka AGF na Absa. Ilikuwa ni katika hafla ya utiaji saini makubaliano hayo jijini Dar es Salaam leo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...
No comments:
Post a Comment