Ikiadhimisha miaka mitano, thamani ya uwekezaji Mfuko wa PSSSF yafikia sh trilioni 7.8 - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Saturday, August 12, 2023

Ikiadhimisha miaka mitano, thamani ya uwekezaji Mfuko wa PSSSF yafikia sh trilioni 7.8

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kiwango cha thamani ya uwekezaji Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) imeongezeka hadi kufikia shilingi trilioni 7.98 kwa mwaka 2022/2023 kutoka shilingi trilioni 7.5 kwa hesabu za mwaka wa fedha ulioishia Juni, 2022.

Amesema hayo leo (Jumamosi, Agosti 12, 2023) wakati wa maadhimisho ya miaka mitano ya mfuko huo na uzinduzi wa huduma za wanachama kidijitali, kwenye ukumbi wa PSSSF jijini Dodoma.

Thamani hii ipo katika soko la hisa ambalo ni kichocheo kikubwa katika ukuaji wa mitaji nchini ambapo mfuko huo ni muwekezaji mkubwa wa ndani mwenye hisa katika makampuni makubwa kama CRDB Bank Plc, NMB Bank Plc, Tanzania Breweries Limited, na Vodacom Tanzania Plc.

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ameitaka Mifuko ya Hifadhi ya jamii kufanya uwekezaji wenye tija kwa wanachama na jamii inayolingana na thamani ya fedha za wanachama “Fanyeni utafiti wa kina kubaini masoko ili uwekezaji unaofanywa usilete hasara kwa mifuko.

Pia, Mheshimiwa Majaliwa ameiagiza mifuko yote ya Hifadhi ya Jamii kuendelea kulipa mafao kwa wakati ili kuleta utulivu kwa wanachama. “Wazee wastaafu wasisumbuliwe, kumbukeni kuwa sisi sote ni wastaafu watarajiwa.

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa ameziagiza taasisi za Serikali kutekeleza agizo la Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alilolitoa wakati uzinduzi wa mkongo wa mawasiliano wa 2Afrika na matumizi ya teknolojia ya 5G la kutaka taasisi zote za Serikali ziwe zinasomana ili kurahisisha na kuboresha utoaji wa huduma kwa Watanzania.

Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof Joyce Ndalichako amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa maono na dhamira ya dhati ya kuimarisha sekta ya hifadhi ya jamii “lengo la Rais Samia ni kuona inafanya kazi kwa tija, ufanisi na kutoa huduma bora."

Tunampongeza pia Mheshimiwa Rais Dkt. Samia kwa uthubutu wa kutoa fedha kwa mfumo wa hati fungani shilingi trilioni 2.17 za kulipa deni ambalo lilimedumu kwa muda mrefu, mfumo huu umewezesha PSSSF kulipa wastaafu kwa wakati.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) CPA Hosea Kashimba amesema kuwa kwa kipindi cha miaka mitano, hadi kufikia Juni, 2023 mfuko huo umelipa kiasi cha shilingi trilioni 8.88 kwa wanufaika 262,095.

Amesema kuwa kati ya Julai, 2018 na Juni, 2023 mfuko huo umeweza kulinda na kuongeza thamani yake kwa asilimia 27.76 kutoka trilioni 5.83 hadi trilioni 8.07 Juni, 2023. “Ongezeko hili ni sawa na wastani wa asilimia 6.72 kwa kila mwaka”.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipokea zawadi kutoka kwa Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako (wa tatu kushoto) wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka mitano ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) pamoja uzinduzi wa huduma za kidigitali za PSSSF Pamoja jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. Huduma zinazopatikana kupitia ‘PSSSF Pamoja’ ni utaratibu wa wanachama wapya kujiunga kwenye mfuko, mfumo wa kidigitali wa kuanzisha madai ya mafao na uhakiki wa wastaafu kupitia simu janja popote walipo bila kufika kwenye ofisi za mfuko. Wengine kutoka kulia ni, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, Mkurugenzi mkuu wa mfuko huo, CPA. Hosea Kashimba na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSSSF, Mhandisi Musa Iyombe.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa huduma za kidigitali ya PSSSF Pamoja, wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka mitano ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) pamoja na uzinduzi wa huduma za kidigitali za mfuko huo jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. Huduma zinazopatikana kupitia PSSSF Pamoja ni utaratibu wa wanachama wapya kujiunga kwenye mfuko, mfumo wa kidigitali wa kuanzisha madai ya mafao na uhakiki wa wastaafu kupitia simu janja popote walipo bila kufika kwenye ofisi za mfuko. Kulia kwa mheshimiwa waziri mkuu kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSSSF, Mhandisi Musa Iyombe na Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, CPA. Hosea Kashimba.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishikana mikono na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), CPA. Hosea Kashimba wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka mitano ya mfuko pamoja na uzinduzi wa PSSSF Pamoja jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa PSSSF, Mhandisi Musa Iyombe na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule. Waziri mkuu Majaliwa ameagiza mifuko yote ya hifadhi ya jamii kulipa mafao kwa wakati.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wa nne kulia), akikabidhi zawadi kwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSSSF, Dk. Aggrey Mlimuka wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka mitano ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) pamoja na uzinduzi wa huduma za kidigitali za PSSSF Pamoja jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wahudhuriaji wakishiriki maadhimisho ya miaka mitano ya miaka mitano ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) pamoja na uzinduzi wa huduma za kidigitali za PSSSF Pamoja jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Wapiga ngoma wakionesha umahiri wao kunogesha sherehe za maadhimisho ya miaka mitano ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, viongozi wa Mfuko wa PSSF, viongozi wa kiserikali wa mkoa wa Dodoma pamoja na wahuduriaji wengine mashuhuri wakipozi kwa picha ya kumbukumnbu mara baada ya maadhimisho ya miaka mitano ya PSSSF mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.

No comments:

Post a Comment

Absa Dar City Marathon 2024 zatimua vumbi jijini Dar es Salaam

Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Bwana Aron Luhanga (kushoto), akikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza wa mbio za nu...

Pages